Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 103:15-22

Zab 103:15-22 SUV

Mwanadamu siku zake zi kama majani; Kama ua la kondeni ndivyo asitawivyo. Maana upepo hupita juu yake, kumbe haliko! Na mahali pake hapatalijua tena. Bali fadhili za BWANA zina wamchao Tangu milele hata milele, Na haki yake ina wana wa wana; Maana, wale walishikao agano lake, Na kuyakumbuka maagizo yake ili wayafanye. BWANA ameweka kiti chake cha enzi mbinguni, Na ufalme wake unavitawala vitu vyote. Mhimidini BWANA, enyi malaika zake, Ninyi mlio hodari, mtendao neno lake, Mkiisikiliza sauti ya neno lake. Mhimidini BWANA, enyi majeshi yake yote, Ninyi watumishi wake mfanyao mapenzi yake. Mhimidini BWANA, enyi matendo yake yote, Mahali pote pa milki yake. Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA.

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Zab 103:15-22