Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 103:15-22

Zaburi 103:15-22 NEN

Kuhusu mwanadamu, siku zake ni kama majani, anachanua kama ua la shambani; upepo huvuma juu yake nalo hutoweka, mahali pake hapalikumbuki tena. Lakini kutoka milele hata milele upendo wa BWANA uko kwa wale wamchao, nayo haki yake kwa watoto wa watoto wao: kwa wale walishikao agano lake na kukumbuka kuyatii mausia yake. BWANA ameweka imara kiti chake cha enzi mbinguni, ufalme wake unatawala juu ya vyote. Mhimidini BWANA, enyi malaika zake, ninyi mlio mashujaa mnaozitii amri zake, ninyi mnaotii neno lake. Mhimidini BWANA, ninyi jeshi lake lote la mbinguni, ninyi watumishi wake mnaofanya mapenzi yake. Mhimidini BWANA, kazi zake zote kila mahali katika milki yake.

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Zaburi 103:15-22