Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ayu 38:12-24

Ayu 38:12-24 SUV

Je! Umeiamuru asubuhi tangu siku zako zilipoanza? Umeyajulisha mapambazuko mahali pake? Yapate kuishika miisho ya nchi, Waovu wakung’utwe wakawe mbali nayo? Hubadilika mfano wa udongo chini ya muhuri, Vitu vyote vinatokea kama mavazi. Na waovu nuru yao huzuiliwa isiwafikie, Na mkono ulioinuka huvunjika. Je! Umeziingia chemchemi za bahari, Au umetembea mahali pa siri pa vilindi? Je! Umefunuliwa malango ya mauti, Au umeyaona malango ya kuzimu? Umeyafahamu mapana ya dunia? Haya! Sema, ikiwa unayajua hayo yote. Iko wapi njia ya kuyafikia makao ya nuru? Na giza pia, mahali pake ni wapi? Upate kuipeleka hata mpaka wake, Upate kuelewa na mapito ya kuiendea nyumba yake? Hukosi unajua, maana ulizaliwa wakati huo, Na hesabu ya siku zako ni kubwa! Je! Umeziingia ghala za theluji, Au umeziona ghala za mvua ya mawe, Nilizoziweka akiba kwa wakati wa misiba, Kwa siku ya mapigano na vita? Je! Nuru hutengwa kwa njia gani, Au upepo wa mashariki hutawanywaje juu ya nchi?