Yobu 38:12-24
Yobu 38:12-24 Biblia Habari Njema (BHN)
“Yobu, tangu uzaliwe umewahi kuamuru kupambazuke? na kulifanya pambazuko lijue mahali pake, ili lipate kuikamata dunia kwa pembe zake na kuwatimulia mbali waovu waliomo? Dunia hugeuka na kupata rangi kama vazi; kama udongo wa mfinyanzi unavyogeuzwa na mhuri. Lakini waovu watanyimwa mwanga wao, mkono wanaonyosha kupiga watu utavunjwa. “Je, umepata kufika kwenye chemchemi za bahari? au kutembea juu ya sakafu ya kilindi cha bahari? Je, umewahi kuoneshwa malango ya kifo, au kuyaona malango ya makazi ya giza nene? Je, wajua ukubwa wa dunia? Niambie kama unajua haya yote. “Je, makao ya mwanga yako wapi? Nyumbani kwa giza ni wapi, ili upate kulipeleka kwenye makao yake, na kuifahamu njia ya kwenda huko kwake. Wewe unapaswa kujua, wewe ambaye umekwisha ishi miaka mingi! “Je, umewahi kuingia katika bohari za theluji, au kuona bohari za mvua ya mawe ambavyo nimevihifadhi kwa ajili ya wakati wa fujo, kwa ajili ya siku ya mapigano na vita? Ipi njia ya kwenda mahali mwanga unapogawanywa, au huko kunakotoka upepo wa mashariki ukasambazwa duniani?
Yobu 38:12-24 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Je! Umeiamuru asubuhi tangu siku zako zilipoanza? Umeyajulisha mapambazuko mahali pake? Yapate kuishika miisho ya nchi, Waovu wakung'utwe wakawe mbali nayo? Hubadilika mfano wa udongo chini ya mhuri, Vitu vyote vinatokea kama mavazi. Na waovu nuru yao huzuiliwa isiwafikie, Na mkono ulioinuka huvunjika. Je! Umeziingia chemchemi za bahari, Au umetembea mahali pa siri pa vilindi? Je! Umefunuliwa malango ya mauti, Au umeyaona malango ya kuzimu? Umeyafahamu mapana ya dunia? Haya! Sema, ikiwa unayajua hayo yote. Iko wapi njia ya kuyafikia makao ya nuru? Na giza pia, mahali pake ni wapi? Upate kuipeleka hata mpaka wake, Upate kuyaelewa mapito ya kuiendea nyumba yake? Hukosi unajua, maana ulizaliwa wakati huo, Na hesabu ya siku zako ni kubwa! Je! Umeziingia ghala za theluji, Au umeziona ghala za mvua ya mawe, Nilizoziweka akiba kwa wakati wa misiba, Kwa siku ya mapigano na vita? Je! Nuru hutengwa kwa njia gani, Au upepo wa mashariki hutawanywaje juu ya nchi?
Yobu 38:12-24 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Je! Umeiamuru asubuhi tangu siku zako zilipoanza? Umeyajulisha mapambazuko mahali pake? Yapate kuishika miisho ya nchi, Waovu wakung’utwe wakawe mbali nayo? Hubadilika mfano wa udongo chini ya muhuri, Vitu vyote vinatokea kama mavazi. Na waovu nuru yao huzuiliwa isiwafikie, Na mkono ulioinuka huvunjika. Je! Umeziingia chemchemi za bahari, Au umetembea mahali pa siri pa vilindi? Je! Umefunuliwa malango ya mauti, Au umeyaona malango ya kuzimu? Umeyafahamu mapana ya dunia? Haya! Sema, ikiwa unayajua hayo yote. Iko wapi njia ya kuyafikia makao ya nuru? Na giza pia, mahali pake ni wapi? Upate kuipeleka hata mpaka wake, Upate kuelewa na mapito ya kuiendea nyumba yake? Hukosi unajua, maana ulizaliwa wakati huo, Na hesabu ya siku zako ni kubwa! Je! Umeziingia ghala za theluji, Au umeziona ghala za mvua ya mawe, Nilizoziweka akiba kwa wakati wa misiba, Kwa siku ya mapigano na vita? Je! Nuru hutengwa kwa njia gani, Au upepo wa mashariki hutawanywaje juu ya nchi?
Yobu 38:12-24 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
“Umepata kuiamrisha asubuhi ipambazuke, au kuyaonesha mapambazuko mahali pake, yapate kushika miisho ya dunia, na kuwakung’uta waovu waliomo? Dunia hubadilika kama udongo wa mfinyanzi chini ya muhuri; sura yake hukaa kama ile ya vazi. Waovu huzuiliwa nuru yao, nao mkono wao ulioinuliwa huvunjwa. “Je, umepata kufika kwenye chemchemi za bahari? Au kutembea mahali pa ndani pa vilindi? Umewahi kuoneshwa malango ya mauti? Umewahi kuiona milango ya uvuli wa mauti? Je, wewe unafahamu ukubwa wa dunia? Niambie kama unajua haya yote. “Njia ya kufika kwenye makao ya nuru ni ipi? Nako maskani mwa giza ni wapi? Je, unaweza kuvirudisha kwenye makao yake? Unajua njia za kufika maskani mwake? Hakika unajua, kwa kuwa ulikuwa umeshazaliwa! Kwani umeishi miaka mingi! “Je, umeshawahi kuingia katika maghala ya theluji, au kuona maghala ya mvua ya mawe, ambazo nimeziweka akiba kwa ajili ya wakati wa taabu, na kwa ajili ya wakati wa vita na mapigano? Njia iendayo mahali miali ya radi inapotawanywa ni ipi, au njia iendayo mahali upepo wa mashariki unaposambazwa juu ya dunia?