Ayu 28:20-28
Ayu 28:20-28 SUV
Basi hekima yatoka wapi? Na mahali pa ufahamu ni wapi? Kwa kuwa imefichwa mbali na macho ya wote walio hai, Na kusitirika na ndege wa angani. Uharibifu na Mauti husema, Tumesikia habari zake kwa masikio yetu. Mungu ndiye aijuaye njia yake, Naye anajua mahali pake. Maana anatazama hata miisho ya nchi, Na kuona chini ya mbingu nzima. Apate kuufanyia upepo uzito wake; Naam, anayapima maji kwa kipimo. Hapo alipoiwekea mvua amri, Na njia kwa umeme wa radi. Ndipo alipoiona na kuitangaza; Aliithibitisha, naam, na kuichunguza. Kisha akamwambia mwanadamu, Tazama, kumcha Bwana ndiyo hekima, Na kujitenga na uovu ndio ufahamu.