Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zekaria 9:14-17

Zekaria 9:14-17 NENO

Kisha Mwenyezi Mungu atawatokea; mshale wake utamulika kama radi. Bwana Mungu Mwenyezi atapiga tarumbeta, naye atatembea katika tufani za kusini, na Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni atawalinda. Wataangamiza na kushinda kwa mawe ya kutupa kwa kombeo. Watakunywa na kunguruma kama waliolewa mvinyo; watajaa kama bakuli linalotumika kunyunyizia kwenye pembe za madhabahu. Mwenyezi Mungu, Mungu wao, atawaokoa siku hiyo kama kundi la watu wake. Watang’ara katika nchi yake kama vito vya thamani kwenye taji. Jinsi gani watavutia na kuwa wazuri! Nafaka itawastawisha vijana wanaume, nayo divai mpya vijana wanawake.