Zekaria 9:14-17
Zekaria 9:14-17 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Naye BWANA ataonekana juu yao, Na mshale wake utatoka kama umeme; Na Bwana MUNGU ataipiga tarumbeta, Naye atakwenda kwa pepo za kisulisuli za kusini. BWANA wa majeshi atawalinda; Nao watakula na kuyakanyaga mawe ya teo; Nao watakunywa na kufanya kelele kama kwa divai; Nao watajazwa kama mabakuli, kama pembe za madhabahu. Na BWANA, Mungu wao, atawaokoa siku hiyo, Kama kundi la watu wake; Kwa maana watakuwa kama vito vya taji, Vikimeta-meta juu ya nchi yake. Maana wema wake, jinsi ulivyo mwingi! Na uzuri wake, jinsi ulivyo mwingi! Nafaka itawasitawisha vijana wanaume, Na divai mpya vijana wanawake.
Zekaria 9:14-17 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Kisha Mwenyezi Mungu atawatokea; mshale wake utamulika kama radi. Bwana Mungu Mwenyezi atapiga tarumbeta, naye atatembea katika tufani za kusini, na Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni atawalinda. Wataangamiza na kushinda kwa mawe ya kutupa kwa kombeo. Watakunywa na kunguruma kama waliolewa mvinyo; watajaa kama bakuli linalotumika kunyunyizia kwenye pembe za madhabahu. Mwenyezi Mungu, Mungu wao, atawaokoa siku hiyo kama kundi la watu wake. Watang’ara katika nchi yake kama vito vya thamani kwenye taji. Jinsi gani watavutia na kuwa wazuri! Nafaka itawastawisha vijana wanaume, nayo divai mpya vijana wanawake.
Zekaria 9:14-17 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu atawatokea watu wake; atafyatua mishale yake kama umeme. Bwana Mwenyezi-Mungu atapiga tarumbeta; atafika pamoja na kimbunga cha kusini. Mwenyezi-Mungu wa majeshi atawalinda watu wake, nao watawaangamiza maadui zao. Watapiga kelele vitani kama walevi wataimwaga damu ya maadui zao. Itatiririka kama damu ya tambiko iliyomiminwa madhabahuni kutoka bakulini. Wakati huo, Mwenyezi-Mungu, Mungu wao, atawaokoa, maana wao ni kundi lake; nao watang'aa katika nchi yake kama mawe ya thamani katika taji. Jinsi gani uzuri na urembo wake ulivyo! Wavulana na wasichana watanawiri kwa wingi wa nafaka na divai mpya.
Zekaria 9:14-17 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Naye BWANA ataonekana juu yao, Na mshale wake utatoka kama umeme; Na Bwana MUNGU ataipiga tarumbeta, Naye atakwenda kwa pepo za kisulisuli za kusini. BWANA wa majeshi atawalinda; Nao watakula na kuyakanyaga mawe ya teo; Nao watakunywa na kufanya kelele kama kwa divai; Nao watajazwa kama mabakuli, kama pembe za madhabahu. Na BWANA, Mungu wao, atawaokoa siku hiyo, Kama kundi la watu wake; Kwa maana watakuwa kama vito vya taji, Vikimetameta juu ya nchi yake. Maana wema wake, jinsi ulivyo mwingi! Na uzuri wake, jinsi ulivyo mwingi! Nafaka itawasitawisha vijana wanaume, Na divai mpya vijana wanawake.