Ufunuo Utangulizi
Utangulizi
Kitabu hiki kinazungumzia Ufunuo wa Isa Al-Masihi aliopewa na Mwenyezi Mungu, ili awaoneshe watumishi wake mambo ambayo yalitarajiwa kutukia karibuni. Ijapokuwa kitabu kimechukua jina la mwandishi, “Ufunuo wa Yohana”, ukweli ni kwamba hakimzungumzii Yohana wala hakimfunui yeye, bali kinamzungumzia na kumfunua Isa Al-Masihi. Isa ndiye Mwana-Kondoo ambaye ameleta ukombozi. Yeye ndiye atakayehukumu na kushinda kabisa uovu, ili ufalme wa milele ulio bora kabisa uthibitishwe.
Mwandishi
Mtume Yohana.
Kusudi
Kuwahimiza waumini kukataa shinikizo la kumwabudu mfalme, na kusimama imara katika majaribu hadi kifo.
Mahali
Kisiwa cha Patmo, karibu na pwani ya Uyunani (Ugiriki).
Tarehe
Mnamo 95 B.K.
Wahusika Wakuu
Yohana na Isa.
Wazo Kuu
Kitabu hiki kinamwonesha Isa kuwa Mwana-Kondoo aliyechinjwa kwa ajili ya dhambi za ulimwengu, na atakavyoleta utawala wa haki milele na milele.
Mambo Muhimu
Kitabu hiki kinatumia lugha ya kiufunuo, yaani matumizi ya mifano, na majina ya kufananisha, ndoto, maono, matumizi makubwa ya tarakimu, na pia viumbe vya mbinguni na vya dunia vya kutisha. Kinaonesha mambo yale Yohana aliyaona, yaani maono ya Isa Al-Masihi akiwa katikati ya kile kinara cha taa. Nayo mambo yaliyopo ina maana zile barua saba kwa makundi saba ya waumini katika sehemu ya Asia Ndogo. Nayo mambo ambayo hayana budi kutukia baada ya hayo inaweza kumaanisha matukio yanayohusu kunyakuliwa kwa waumini wa Isa au siku za mwisho.
Yaliyomo
Mwanzo wa maono kuhusu Isa Al-Masihi (1:1-20)
Barua kwa makundi saba ya waumini (2:1–3:22)
Maono kuhusu Mwenyezi Mungu na Mwana-Kondoo (4:1–5:14)
Mihuri saba ya hukumu (6:1–8:5)
Tarumbeta saba za hukumu (8:6–11:19)
Maono kuhusu vita ya duniani na mbinguni (12:1–14:20)
Mabakuli saba ya hukumu (15:1–16:21)
Hukumu juu ya Kahaba Babeli (17:1–19:21)
Mwisho wa nyakati, na wakati ujao (20:1–22:21).
Iliyochaguliwa sasa
Ufunuo Utangulizi: NENO
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
![None](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2F58%2Fhttps%3A%2F%2Fweb-assets.youversion.com%2Fapp-icons%2Fsw.png&w=128&q=75)
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Neno: Maandiko Matakatifu™ NMM™
Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc.
Imetumiwa kwa ruhusa.
Haki zote zimehifadhiwa duniani kote.
Kiswahili Contemporary Scriptures™
Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Used with permission. All rights reserved worldwide.