Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 88:1-5

Zaburi 88:1-5 NENO

Ee BWANA, Mungu uniokoaye, nimelia mbele zako usiku na mchana. Maombi yangu yafike mbele zako, utegee kilio changu sikio lako. Kwa maana nafsi yangu imejaa taabu, na maisha yangu yanakaribia kaburi. Nimehesabiwa miongoni mwa wale wanaoshuka shimoni; niko kama mtu asiye na nguvu. Nimetengwa pamoja na wafu, kama waliochinjwa walalao kaburini, ambao huwakumbuki tena, ambao wamekatiliwa mbali na uangalizi wako.