Zaburi 88:1-5
Zaburi 88:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)
Ee Mwenyezi-Mungu, mwokozi wangu, ninalia mchana kutwa, na usiku nakulalamikia. Sala yangu ikufikie, usikilize kilio changu. Maafa mengi yamenipata, nami niko karibu kufa. Ninaonekana kama mtu anayekufa, nguvu zangu zote zimeniishia. Nimesahauliwa kati ya wafu, kama waliouawa, walioko kaburini; kama wale ambao huwakumbuki tena, ambao wametengwa na ulinzi wako.
Zaburi 88:1-5 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ee BWANA, Mungu wa wokovu wangu Mchana na usiku nimelia mbele zako. Maombi yangu yafike mbele zako, Ukitegee kilio changu sikio lako. Maana nafsi yangu imeshiba taabu, Na uhai wangu umekaribia kuzimu. Nimehesabiwa pamoja nao washukao shimoni; Nimekuwa kama mtu asiye na msaada. Miongoni mwao waliokufa nimetupwa, Kama waliouawa walalao makaburini. Hao ambao Wewe huwakumbuki tena, Wametengwa mbali na mkono wako.
Zaburi 88:1-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ee BWANA, Mungu wa wokovu wangu Mchana na usiku nimelia mbele zako. Maombi yangu yafike mbele zako, Uutegee ukelele wangu sikio lako. Maana nafsi yangu imeshiba taabu, Na uhai wangu umekaribia kuzimu. Nimehesabiwa pamoja nao washukao shimoni; Nimekuwa kama mtu asiye na msaada. Miongoni mwao waliokufa nimetupwa, Kama waliouawa walalao makaburini. Hao ambao Wewe huwakumbuki tena, Wametengwa mbali na mkono wako.
Zaburi 88:1-5 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Ee Mwenyezi Mungu, Mungu uniokoaye, nimelia mbele zako usiku na mchana. Maombi yangu yafike mbele zako, utegee kilio changu sikio lako. Kwa maana nafsi yangu imejaa taabu, na maisha yangu yanakaribia kaburi. Nimehesabiwa miongoni mwa wale wanaoshuka shimoni; niko kama mtu asiye na nguvu. Nimetengwa pamoja na wafu, kama waliochinjwa walalao kaburini, ambao huwakumbuki tena, ambao wamekatiliwa mbali na uangalizi wako.