Zaburi 59:1-9
Zaburi 59:1-9 NENO
Ee Mungu, uniokoe na adui zangu, unilinde kutokana na hao wanaoinuka dhidi yangu. Uniponye na watu watendao maovu, uniokoe kutokana na wanaomwaga damu. Tazama wanavyonivizia! Watu wakali wananifanyia hila, ingawa Ee Mwenyezi Mungu, mimi sijakosea wala kutenda dhambi. Sijatenda kosa; hata hivyo wako tayari kunishambulia. Inuka unisaidie, uone hali yangu mbaya! Ee Mungu, Bwana Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, uliye Mungu wa Israeli, zinduka uyaadhibu mataifa yote; usioneshe huruma kwa wasaliti waovu. Hurudi wakati wa jioni, wakibweka kama mbwa, wakiuzurura mji. Tazama yale wanayotema kutoka vinywa vyao, hutema panga kutoka midomo yao, nao husema, “Ni nani atakayetusikia?” Lakini wewe, Mwenyezi Mungu, uwacheke; unayadharau mataifa hayo yote. Ee nguvu yangu, ninakutazama wewe, wewe, Ee Mungu, ndiwe ngome yangu