Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 55:4-8

Zaburi 55:4-8 NEN

Moyo wangu umejaa uchungu, hofu ya kifo imenishambulia. Woga na kutetemeka vimenizunguka, hofu kuu imenigharikisha. Nilisema, “Laiti ningekuwa na mbawa za njiwa! Ningeruka niende mbali kupumzika. Ningalitorokea mbali sana na kukaa jangwani, ningaliharakisha kwenda mahali pa salama, mbali na tufani kali na dhoruba.”