Zaburi 5:11-12
Zaburi 5:11-12 NENO
Lakini wote wanaokimbilia kwako na wafurahi, waimbe kwa shangwe daima. Ueneze ulinzi wako juu yao, ili wale wanaolipenda jina lako wapate kukushangilia. Kwa hakika, Ee Mwenyezi Mungu, unawabariki wenye haki, unawazunguka kwa wema wako kama ngao.