Zaburi 5:11-12
Zaburi 5:11-12 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Lakini wote wanaokimbilia kwako na wafurahi, waimbe kwa shangwe daima. Ueneze ulinzi wako juu yao, ili wale wanaolipenda jina lako wapate kukushangilia. Kwa hakika, Ee Mwenyezi Mungu, unawabariki wenye haki, unawazunguka kwa wema wako kama ngao.
Zaburi 5:11-12 Biblia Habari Njema (BHN)
Lakini wafurahi wote wanaokimbilia usalama kwako, waimbe kwa shangwe daima. Uwalinde wanaolipenda jina lako, wapate kushangilia kwa sababu yako. Maana wewe Mwenyezi-Mungu wawabariki waadilifu; wawakinga kwa fadhili zako kama kwa ngao.
Zaburi 5:11-12 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nao wote wanaokukimbilia watafurahi; Watapiga kelele za furaha daima. Kwa kuwa Wewe unawahifadhi, Walipendao jina lako watakufurahia. Kwa maana Wewe utambariki mwenye haki; BWANA, utamzungushia radhi kama ngao.
Zaburi 5:11-12 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nao wote wanaokukimbilia watafurahi; Watapiga daima kelele za furaha. Kwa kuwa Wewe unawahifadhi, Walipendao jina lako watakufurahia. Kwa maana Wewe utambariki mwenye haki; BWANA, utamzungushia radhi kama ngao.