Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 4:1-8

Zaburi 4:1-8 NENO

Nijibu nikuitapo, Ee Mungu wangu mwenye haki! Nipumzishe katika shida zangu; nirehemu, usikie ombi langu. Enyi watu, mtabadilisha utukufu wangu kuwa aibu hadi lini? Mtapenda udanganyifu na kufuata miungu ya uongo hadi lini? Fahamuni hakika kwamba Mwenyezi Mungu amewatenga wale wamchao kwa ajili yake; Mwenyezi Mungu atanisikia nimwitapo. Katika hasira yako, usitende dhambi. Tulieni kimya mkiwa vitandani mwenu, mkiichunguza mioyo yenu. Toeni dhabihu zilizo haki; mtegemeeni Mwenyezi Mungu. Wengi wanauliza, “Ni nani awezaye kutuonesha jema lolote?” Ee Mwenyezi Mungu, tuangazie nuru ya uso wako. Wewe umejaza moyo wangu kwa furaha kubwa kuliko watu waliopata nafaka na divai kwa wingi. Nitajilaza chini na kulala kwa amani, kwa kuwa wewe peke yako, Ee Mwenyezi Mungu, waniwezesha kukaa kwa salama.