Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 25:11-22

Zaburi 25:11-22 NEN

Ee BWANA, kwa ajili ya jina lako, unisamehe uovu wangu, ijapokuwa ni mwingi. Ni nani basi, mtu yule anayemcha BWANA? Atamfundisha katika njia atakayoichagua kwa ajili yake. Mtu huyo atafanikiwa maishani mwake, nao wazao wake watairithi nchi. Siri ya BWANA iko kwa wale wamchao, yeye huwajulisha agano lake. Macho yangu humwelekea BWANA daima, kwa kuwa yeye peke yake ndiye ataitoa miguu yangu kutoka mtego. Nigeukie na unihurumie, kwa maana mimi ni mpweke na mwenye kuteseka. Shida za moyo wangu zimeongezeka, niokoe katika dhiki yangu. Uangalie mateso na shida zangu na uniondolee dhambi zangu zote. Tazama adui zangu walivyo wengi, pia uone jinsi wanavyonichukia vikali! Uyalinde maisha yangu na uniokoe, usiniache niaibike, kwa maana nimekukimbilia wewe. Uadilifu na uaminifu vinilinde, kwa sababu tumaini langu ni kwako. Ee Mungu, wakomboe Israeli, katika shida zao zote!