Zaburi 25:1-3
Zaburi 25:1-3 NEN
Kwako wewe, Ee BWANA, nainua nafsi yangu, ni wewe ninayekutumainia, Ee Mungu wangu. Usiniache niaibike, wala usiache adui zangu wakanishinda. Kamwe hakuna hata mmoja anayekutegemea atakayeaibishwa, bali wataaibishwa wafanyao hila bila sababu.