Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 20

20
Zaburi 20
Maombi kwa ajili ya ushindi
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.
1Mwenyezi Mungu na akujibu unapokuwa katika dhiki,
jina la Mungu wa Yakobo na liwe kinga yako.
2Na akutumie msaada kutoka patakatifu
na akupatie msaada kutoka Sayuni.
3Na azikumbuke dhabihu zako zote,
na azikubali sadaka zako za kuteketezwa.
4Na akujalie haja ya moyo wako,
na aifanikishe mipango yako yote.
5Tutashangilia kwa furaha utakaposhinda,
tutainua bendera zetu kwa jina la Mungu wetu.
Mwenyezi Mungu na akupe haja zako zote.
6Sasa nafahamu kuwa Mwenyezi Mungu
humwokoa mpakwa mafuta wake,
humjibu kutoka mbingu yake takatifu
kwa nguvu za wokovu wa mkono wake wa kuume.
7Wengine wanatumaini magari ya vita, na wengine farasi,
bali sisi tutalitumainia jina la Mwenyezi Mungu, Mungu wetu.
8Wao wameshushwa chini na kuanguka,
bali sisi tunainuka na kusimama imara.
9Ee Mwenyezi Mungu, mwokoe mfalme!
Tujibu tunapokuita!

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 20: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia