Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 145:11-21

Zaburi 145:11-21 NEN

Watasimulia utukufu wa ufalme wako na kusema juu ya ukuu wako, ili watu wote wajue matendo yako makuu na utukufu wa fahari ya ufalme wako. Ufalme wako ni ufalme wa milele, mamlaka yako hudumu vizazi vyote. BWANA ni mwaminifu kwa ahadi zake zote na mwenye upendo kwa vyote alivyovifanya. BWANA huwategemeza wote waangukao, na huwainua wote waliolemewa na mizigo yao. Macho yao wote yanakutazama wewe, nawe huwapa chakula chao wakati wake. Waufumbua mkono wako, watosheleza haja ya kila kitu kilicho hai. BWANA ni mwenye haki katika njia zake zote, na mwenye upendo kwa vyote alivyovifanya. BWANA yu karibu na wote wamwitao, karibu na wote wamwitao kwa uaminifu. Huwatimizia wamchao matakwa yao, husikia kilio chao na kuwaokoa. BWANA huwalinda wote wampendao, bali waovu wote atawaangamiza. Kinywa changu kitazinena sifa za BWANA. Kila kiumbe na kilisifu jina lake takatifu milele na milele.