Zaburi 145:11-21
Zaburi 145:11-21 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Wataunena utukufu wa ufalme wako, Na kuuhadithia uweza wako. Ili kuwajulisha watu matendo yake makuu, Na utukufu wa fahari ya ufalme wake. Ufalme wako ni ufalme wa zamani zote, Na mamlaka yako ni ya vizazi vyote. BWANA huwategemeza wote waangukao, Huwainua wote walioinama chini. Macho ya watu wote yakuelekea Wewe, Nawe huwapa chakula chao wakati wake. Waufumbua mkono wako, Wakishibisha kila kilicho hai matakwa yake. BWANA ni mwenye haki katika njia zake zote, Na mwenye fadhili juu ya kazi zake zote. BWANA yu karibu na wote wamwitao, Wote wamwitao kwa uaminifu. Atawafanyia wamchao matakwa yao, Naye atakisikia kilio chao na kuwaokoa. BWANA huwahifadhi wote wampendao, Na wote wasio haki atawaangamiza. Kinywa changu kitazinena sifa za BWANA; Wote wenye mwili na walihimidi jina lake takatifu milele na milele.
Zaburi 145:11-21 Biblia Habari Njema (BHN)
Watasema juu ya utukufu wa ufalme wako, na kutangaza juu ya nguvu yako kuu, ili kila mtu ajue matendo yako makuu, na fahari tukufu ya ufalme wako. Ufalme wako ni ufalme wa milele; mamlaka yako yadumu vizazi vyote. Mwenyezi-Mungu ni mwaminifu katika ahadi zake zote, ni mwema katika matendo yake yote. Mwenyezi-Mungu huwategemeza wote wanaoanguka; huwainua wote waliokandamizwa. Viumbe vyote vinakutazama kwa hamu, nawe wavipa chakula chao kwa wakati wake. Waufumbua mkono wako kwa ukarimu, watosheleza mahitaji ya kila kiumbe hai. Mwenyezi-Mungu ni mwadilifu katika njia zake zote; ni mwema katika matendo yake yote. Mwenyezi-Mungu yuko karibu na wote wanaomwomba, wote wanaomwomba kwa moyo mnyofu. Huwapatia mahitaji yao wote wanaomcha; husikia kilio chao na kuwaokoa. Mwenyezi-Mungu huwalinda wote wanaompenda; lakini atawaangamiza waovu wote. Nitatangaza sifa za Mwenyezi-Mungu; viumbe vyote vilisifu jina lake takatifu, milele na milele.
Zaburi 145:11-21 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Wataunena utukufu wa ufalme wako, Na kusena uweza wako. Ili kuwajulisha watu matendo yake makuu, Na utukufu wa fahari ya ufalme wake. Ufalme wako ni ufalme wa milele, BWANA ni mwaminifu katika maneno yake yote, Na mwenye fadhili katika matendo yake yote Na mamlaka yako ni ya vizazi vyote. BWANA huwategemeza wote waangukao, Huwainua wote walioinama chini. Macho ya watu wote yakuelekea Wewe, Nawe huwapa chakula chao wakati wake. Waufumbua mkono wako, Wakishibisha kila kilicho hai matakwa yake. BWANA ni mwenye haki katika njia zake zote, Na mwenye huruma katika matendo yake yote. BWANA yuko karibu na wote wamwitao, Wote wamwitao kwa uaminifu. Hutimiza matakwa ya wote wamchao, Na pia husikia kilio chao, na huwaokoa. BWANA huwahifadhi wote wampendao, Na wote wasio haki atawaangamiza. Kinywa changu kitazinena sifa za BWANA; Wote wenye mwili na walihimidi jina lake takatifu milele na milele.
Zaburi 145:11-21 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Watasimulia utukufu wa ufalme wako na kusema juu ya ukuu wako, ili watu wote wajue matendo yako makuu na utukufu wa fahari ya ufalme wako. Ufalme wako ni ufalme wa milele, mamlaka yako hudumu vizazi vyote. BWANA ni mwaminifu kwa ahadi zake zote na mwenye upendo kwa vyote alivyovifanya. BWANA huwategemeza wote waangukao, na huwainua wote waliolemewa na mizigo yao. Macho yao wote yanakutazama wewe, nawe huwapa chakula chao wakati wake. Waufumbua mkono wako, watosheleza haja ya kila kitu kilicho hai. BWANA ni mwenye haki katika njia zake zote, na mwenye upendo kwa vyote alivyovifanya. BWANA yu karibu na wote wamwitao, karibu na wote wamwitao kwa uaminifu. Huwatimizia wamchao matakwa yao, husikia kilio chao na kuwaokoa. BWANA huwalinda wote wampendao, bali waovu wote atawaangamiza. Kinywa changu kitazinena sifa za BWANA. Kila kiumbe na kilisifu jina lake takatifu milele na milele.