Zaburi 115
115
Zaburi 115
Mwenyezi Mungu Mmoja wa kweli
1Sio kwetu sisi, Ee Mwenyezi Mungu, sio kwetu sisi,
bali utukufu ni kwa jina lako,
kwa sababu ya upendo
na uaminifu wako.
2Kwa nini mataifa waseme,
“Yuko wapi Mungu wao?”
3Mungu wetu yuko mbinguni,
naye hufanya lolote limpendezalo.
4Lakini sanamu zao ni za fedha na dhahabu,
zilizotengenezwa kwa mikono ya wanadamu.
5Zina vinywa, lakini haziwezi kusema,
zina macho, lakini haziwezi kuona;
6zina masikio, lakini haziwezi kusikia,
zina pua, lakini haziwezi kunusa;
7zina mikono, lakini haziwezi kupapasa,
zina miguu, lakini haziwezi kutembea;
wala koo zao haziwezi kutoa sauti.
8Wale wanaozitengeneza watafanana nazo,
vivyo hivyo wale wote wanaozitumainia.
9Ee nyumba ya Israeli, mtumainini Mwenyezi Mungu,
yeye ni msaada na ngao yao.
10Ee nyumba ya Haruni, mtumainini Mwenyezi Mungu,
yeye ni msaada na ngao yao.
11Ninyi mnaomcha, mtumainini Mwenyezi Mungu,
yeye ni msaada na ngao yao.
12Mwenyezi Mungu anatukumbuka na atatubariki:
ataibariki nyumba ya Israeli,
ataibariki nyumba ya Haruni,
13atawabariki wale wanaomcha Mwenyezi Mungu,
wadogo kwa wakubwa.
14Mwenyezi Mungu na awawezeshe kuongezeka,
ninyi na watoto wenu.
15Mbarikiwe na Mwenyezi Mungu
Muumba wa mbingu na dunia.
16Mbingu zilizo juu sana ni mali ya Mwenyezi Mungu,
lakini dunia amempa mwanadamu.
17Sio wafu wanaomsifu Mwenyezi Mungu,
wale wanaoshuka mahali pa kimya#115:17 mahali pa kimya maana yake Kuzimu; kwa Kiebrania ni Sheol.,
18bali ni sisi tunaomtukuza Mwenyezi Mungu,
sasa na hata milele.
Msifuni Mwenyezi Mungu.#115:18 kwa Kiebrania ni Hallelu Yah.
Iliyochaguliwa sasa
Zaburi 115: NENO
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Neno: Maandiko Matakatifu™ NMM™
Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc.
Imetumiwa kwa ruhusa.
Haki zote zimehifadhiwa duniani kote.
Kiswahili Contemporary Scriptures™
Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Used with permission. All rights reserved worldwide.