Mithali 26:17-21
Mithali 26:17-21 NENO
Kama yeye amkamataye mbwa kwa masikio, ndivyo alivyo mtu apitaye njiani na kujiingiza kwenye ugomvi usiomhusu. Kama mwendawazimu atupaye mishale ya moto ya kufisha, ndivyo alivyo mtu amdanganyaye jirani yake na kusema, “Nilikuwa nikifanya mzaha tu!” Bila kuni moto huzimika; pasipo uchongezi ugomvi humalizika. Kama makaa juu ya makaa yanayowaka, na kama kuni kwenye moto, ndivyo alivyo mtu mgomvi kwa kuchochea ugomvi.