Hesabu Utangulizi
Utangulizi
Kitabu cha Hesabu kimepewa jina hili kutokana na matukio mawili ya kuwahesabu Waisraeli: La kwanza huko Sinai katika mwaka wa pili baada ya kutoka Misri (Hesabu 1), na la pili huko Yordani katika mwaka wa arobaini (Hesabu 26). Jina la kitabu hiki kwa Kiebrania ni “Bemidbar,” ambalo maana yake ni “Huko jangwani,” jina linaloeleza zaidi mambo yaliyomo.
Kitabu hiki kinatoa maelezo ya safari ya Waisraeli ya miaka 38 wakati walikuwa wanatangatanga jangwani baada ya kuanzishwa kwa Agano la Mwenyezi Mungu katika Mlima Sinai. Kitabu cha Hesabu kinagusia safari ya Waisraeli kutoka Mlima Sinai hadi nchi tambarare ya Moabu katika mpaka wa Kanaani. Kitabu hiki kinaelezea vile Waisraeli walivyonung’unika na kumwasi Mwenyezi Mungu, na hukumu iliyofuata baadaye. Watu wazima waliotoka Misri walikosa nafasi ya kuingia katika Nchi ya Ahadi, isipokuwa watoto wao.
Mwandishi
Musa.
Kusudi
Kuelezea jinsi Waisraeli walivyojitayarisha kuingia katika Nchi ya Ahadi, na walivyoasi na kuhukumiwa.
Mahali
Kitabu hiki kiliandikwa wakati Waisraeli walikuwa wanatangatanga jangwani, mahali fulani katika Ghuba ya Sinai.
Tarehe
Mnamo 1450–1410 K.K.
Wahusika Wakuu
Musa, Haruni, Miriamu, Yoshua, Kalebu, Eleazari, Kora, Balaamu na Balaki.
Wazo Kuu
Kitabu hiki kinaeleza juu ya utunzaji na uongozi wa Mwenyezi Mungu, uvumilivu wake, na uasi wa watu wa Mwenyezi Mungu na matokeo yake. Jambo moja lililokuwa dhahiri na ambalo limerudiwa mara kwa mara katika kitabu chote ni jinsi mkono wa Mwenyezi Mungu ulivyokuwa pamoja na Waisraeli saa zote ili kuwahudumia na kuwapa mahitaji yao.
Mambo Muhimu
Kuhesabiwa kwa Waisraeli, uasi dhidi ya Mwenyezi Mungu, na hukumu ya Waisraeli ya kutangatanga jangwani.
Yaliyomo
Watu kuhesabiwa, mpangilio wa kambi, na kuendelea na safari (1:1–10:10)
Kutoka Sinai hadi nchi tambarare ya Moabu, viongozi kuasi Mwenyezi Mungu (10:11–21:35)
Balaamu, Balaki na Israeli (22:1–25:18)
Kuhesabu watu mara ya pili, na Yoshua kuchukua nafasi ya Musa (26:1–27:23)
Maagizo mbalimbali (28:1–31:54).
Maelekezo kuhusu kuitwaa nchi ya Kanaani (32:1–36:13).
Iliyochaguliwa sasa
Hesabu Utangulizi: NENO
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
![None](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2F58%2Fhttps%3A%2F%2Fweb-assets.youversion.com%2Fapp-icons%2Fsw.png&w=128&q=75)
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Neno: Maandiko Matakatifu™ NMM™
Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc.
Imetumiwa kwa ruhusa.
Haki zote zimehifadhiwa duniani kote.
Kiswahili Contemporary Scriptures™
Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Used with permission. All rights reserved worldwide.