Walawi 27
27
Kukomboa kile kilicho cha Mwenyezi Mungu
1Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, 2“Sema na Waisraeli uwaambie: ‘Kama mtu yeyote ataweka nadhiri maalum ili kuweka watu wakfu kwa Mwenyezi Mungu, kwa kutoa kiasi cha thamani inayolingana, 3thamani ya kukomboa mwanaume mwenye kati ya umri wa miaka ishirini na miaka sitini itakuwa shekeli hamsini#27:3 Shekeli 50 za fedha ni sawa na gramu 600. za fedha, kulingana na shekeli ya mahali patakatifu; 4ikiwa ni mwanamke, weka thamani yake kwa shekeli thelathini#27:4 Shekeli 30 za fedha ni sawa na gramu 360.. 5Kama ni mtu mwenye umri wa miaka kati ya mitano na ishirini, weka thamani ya mwanaume kuwa shekeli ishirini#27:5 Shekeli 20 za fedha ni sawa na gramu 240., na mwanamke shekeli kumi#27:5 Shekeli 10 za fedha ni sawa na gramu 120.. 6Kama ni mtu mwenye umri kati ya mwezi mmoja na miaka mitano, weka thamani ya mwanaume kuwa shekeli tano za fedha, na ile ya mwanamke kuwa shekeli tatu#27:6 Shekeli tatu za fedha ni sawa na gramu 36. za fedha. 7Kama ni mtu mwenye miaka sitini na zaidi, weka thamani ya mwanaume kuwa shekeli kumi na tano#27:7 Shekeli 15 za fedha ni sawa na gramu 180., na mwanamke shekeli kumi. 8Kama mtu yeyote anayeweka nadhiri ni maskini mno kuweza kulipa kiasi kilichowekwa, atampeleka huyo mtu kwa kuhani, ambaye ataweka thamani yake kulingana na kile yule anayeweka nadhiri anaweza kulipa.
9“ ‘Kama kile mtu alichokiwekea nadhiri ni mnyama anayekubalika kama sadaka kwa Mwenyezi Mungu, mnyama huyo aliyetolewa kwa Mwenyezi Mungu anakuwa mtakatifu. 10Mtu haruhusiwi kumbadilisha au kutoa mnyama mzuri kwa mbaya, au mnyama mbaya kwa mzuri. Kama atatoa mnyama badala ya mwingine, wanyama wote wawili, yaani yule aliyetolewa na yule aliyebadiliwa, ni watakatifu. 11Kama alichokiwekea nadhiri ni mnyama aliye najisi, yaani yule asiyekubalika kuwa sadaka kwa Mwenyezi Mungu, huyo mnyama lazima aletwe kwa kuhani, 12ambaye ataamua ubora wa mnyama huyo, kama ni mzuri au mbaya. Thamani yoyote atakayoweka kuhani, hivyo ndivyo itakavyokuwa. 13Kama mwenye mnyama atapenda kumkomboa mnyama huyo, lazima aongeze sehemu ya tano ya thamani yake.
14“ ‘Kama mtu ataweka nyumba yake wakfu kama kitu kitakatifu kwa Mwenyezi Mungu, kuhani ataamua ubora wa nyumba hiyo, kama ni nzuri au mbaya. Thamani yoyote kuhani atakayoweka, basi hivyo ndivyo itakavyokuwa. 15Kama mtu aliyeweka nyumba yake wakfu ataikomboa, lazima aongeze sehemu ya tano ya thamani yake, nayo nyumba itakuwa yake tena.
16“ ‘Ikiwa mtu ataweka sehemu ya ardhi ya jamaa yake wakfu kwa Mwenyezi Mungu, thamani yake itawekwa kulingana na kiasi cha mbegu inayohitajiwa kupandwa katika ardhi hiyo, yaani homeri#27:16 Homeri moja ni sawa na efa 10, ambazo ni sawa na kilo 100. moja ya mbegu za shayiri kwa shekeli hamsini za fedha. 17Akiweka shamba lake wakfu katika Mwaka wa Yubile, ile thamani iliyokwisha wekwa itakuwa hiyo hiyo. 18Lakini akiliweka shamba lake wakfu baada ya Yubile, kuhani ataweka thamani kulingana na idadi ya miaka iliyobaki kufikia Mwaka wa Yubile unaofuata, na thamani yake iliyoamuliwa itapunguzwa. 19Kama mtu anayeweka wakfu shamba anataka kulikomboa, lazima aongeze sehemu ya tano ya thamani yake, nalo shamba litakuwa lake tena. 20Kama pengine halikomboi shamba hilo, au kama ameliuza kwa mtu mwingine, kamwe haliwezi kukombolewa. 21Shamba hilo litakapoachiwa Mwaka wa Yubile, litakuwa takatifu, kama shamba lililotolewa kwa Mwenyezi Mungu, nalo litakuwa mali ya makuhani.
22“ ‘Kama mtu ameweka wakfu kwa Mwenyezi Mungu shamba alilonunua, ambalo si sehemu ya ardhi ya jamaa yake, 23kuhani ataamua thamani yake hadi Mwaka wa Yubile, naye huyo mtu lazima alipe thamani yake siku hiyo kama kitu kitakatifu kwa Mwenyezi Mungu. 24Katika Mwaka wa Yubile, shamba litarudishwa kwa mtu yule ambaye lilinunuliwa kutoka kwake, yule ambaye ardhi ilikuwa mali yake. 25Kila thamani lazima iwekwe kulingana na shekeli ya mahali patakatifu#27:25 Shekeli moja ya mahali patakatifu ni sawa na gramu 11.: gera ishirini kwa shekeli.
26“ ‘Hata hivyo, hakuna mtu atakayemweka wakfu mzaliwa wa kwanza wa mnyama, kwa kuwa mzaliwa wa kwanza tayari ni mali ya Mwenyezi Mungu; awe ng’ombe au kondoo, ni wa Mwenyezi Mungu. 27Kama ni mmoja wa wanyama walio najisi, aweza kumnunua kwa bei iliyowekwa, akiongeza sehemu ya tano ya thamani yake. Kama hatamkomboa, mnyama huyo atauzwa kwa bei iliyowekwa.
28“ ‘Lakini chochote kile mtu alicho nacho na akakiweka wakfu#27:28 akakiweka wakfu ina maana ya kumpa Mwenyezi Mungu kabisa, daima, bila kurudiwa. kwa Mwenyezi Mungu, iwe ni binadamu, au mnyama, au ardhi ya jamaa, hakiwezi kuuzwa au kukombolewa. Chochote kilichowekwa wakfu ni kitakatifu sana kwa Mwenyezi Mungu.
29“ ‘Mtu yeyote aliyewekwa wakfu ili kuangamizwa, hawezi kukombolewa. Mtu kama huyo lazima auawe.
30“ ‘Zaka ya kila kitu kutoka shambani, iwe ni nafaka kutoka kwa ardhi, au tunda kutoka kwa miti, ni mali ya Mwenyezi Mungu; ni takatifu kwa Mwenyezi Mungu. 31Kama mtu akikomboa chochote cha zaka yake, lazima aongeze sehemu ya tano ya thamani yake. 32Zaka yote ya kundi la ng’ombe au la kondoo na mbuzi, kila mnyama wa kumi apitaye chini ya fimbo ya yule awachungaye, atakuwa kitu kitakatifu kwa Mwenyezi Mungu. 33Yule mnyama wa kumi hatachaguliwa kwa kigezo cha uzuri au ubaya, naye haruhusiwi kubadiliwa. Akimbadili, basi mnyama yule wa kwanza na huyo aliyebadiliwa wote watahesabiwa kuwa watakatifu, na haiwezekani kuwakomboa.’ ”
34Haya ndio maagizo Mwenyezi Mungu aliyompa Musa juu ya Mlima Sinai kwa ajili ya Waisraeli.
Iliyochaguliwa sasa
Walawi 27: NENO
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
![None](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2F58%2Fhttps%3A%2F%2Fweb-assets.youversion.com%2Fapp-icons%2Fsw.png&w=128&q=75)
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Neno: Maandiko Matakatifu™ NMM™
Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc.
Imetumiwa kwa ruhusa.
Haki zote zimehifadhiwa duniani kote.
Kiswahili Contemporary Scriptures™
Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Used with permission. All rights reserved worldwide.