Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mathayo 26:6-10

Mathayo 26:6-10 NEN

Yesu alikuwa Bethania nyumbani mwa Simoni aliyekuwa na ukoma, naye mwanamke mmoja akamjia akiwa na chupa ya marhamu yenye manukato ya thamani kubwa; akayamimina kichwani mwa Yesu alipokuwa ameketi mezani kula chakula. Lakini wanafunzi wake walipoona hayo wakakasirika, wakasema, “Upotevu huu wote ni wa nini? Manukato haya yangeuzwa kwa bei kubwa, na fedha hizo wakapewa maskini.” Yesu, akijua jambo hili, akawaambia, “Mbona mnamsumbua huyu mwanamke? Yeye amenitendea jambo zuri sana.

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Mathayo 26:6-10