Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ayubu 39:1-12

Ayubu 39:1-12 NENO

“Je, unajua wakati mbuzi wa mlimani wanapozaa? Je, unatambua wakati kulungu jike anapozaa mtoto wake? Je, unaweza kuhesabu miezi hadi wanapozaa? Je, unajua majira yao ya kuzaa? Wao hujiinamisha na kuzaa watoto wao; uchungu wa kuzaa unakoma. Watoto wao hustawi na kuongezeka nguvu nyikani; huenda zao wala hawarudi tena. “Ni nani aliyemwachia punda-mwitu awe huru? Ni nani aliyezifungua kamba zake? Nimempa nchi isiyokaliwa na watu kuwa masikani yake, nchi ya chumvi kuwa makao yake. Huzicheka ghasia za mji, wala hasikii kelele za mwendesha gari. Huzunguka vilimani kwa ajili ya malisho na kutafuta kila kitu kibichi. “Je, nyati atakubali kukutumikia? Atakaa karibu na hori lako usiku? Je, unaweza kumfungia kwenye matuta kwa kamba? Je, atalima mabonde nyuma yako? Je, utamtumainia kwa ajili ya nguvu zake nyingi? Utamwachia yeye kazi zako nzito? Utaweza kumwamini akuletee nafaka yako nyumbani kutoka shambani na kuikusanya kwenye sakafu yako ya kupuria?