Yobu 39:1-12
Yobu 39:1-12 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Je! Wajua majira ya kuzaa kwao mbuzi-mwitu walio majabalini? Au waweza kusema majira ya kuzaa kwa kulungu? Je! Waweza kuhesabu miezi yao watakayoitimiza? Au waweza kusema majira ya kuzaa kwa kulungu? Wao hujiinamisha, kuzaa watoto wao, Watupa taabu zao. Watoto wao wako katika hali nzuri, hukua katika bara wazi; Huenda zao, wala hawarudi tena. Ni nani aliyemwacha pundamilia aende huru? Au je! Ni nani aliyemfungulia vifungo punda mwitu? Ambaye nimeifanya nyika kuwa nyumba yake, Na nchi ya chumvi kuwa makao yake. Yeye hudharau mshindo wa mji, Wala hasikii kelele zake msimamizi. Upana wa milima ni malisho yake, Hutafutatafuta kila kitu kilicho kibichi. Je! Nyati atakubali kukutumikia? Au atakaa katika zizi lako? Je! Waweza kumfunga nyati kwa kamba matutani? Au, yeye atayalima mabonde nyuma yako? Je! Utamtumaini kwa sababu ana nguvu nyingi? Au, utamwachia yeye kazi yako? Je! Utamtumaini kwamba ataileta mbegu yako nyumbani. Na kukusanya nafaka ya kiwanja chako cha kupuria?
Yobu 39:1-12 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
“Je, unajua wakati mbuzi wa mlimani wanapozaa? Je, unatambua wakati kulungu jike anapozaa mtoto wake? Je, unaweza kuhesabu miezi hadi wanapozaa? Je, unajua majira yao ya kuzaa? Wao hujiinamisha na kuzaa watoto wao; uchungu wa kuzaa unakoma. Watoto wao hustawi na kuongezeka nguvu nyikani; huenda zao wala hawarudi tena. “Ni nani aliyemwachia punda-mwitu awe huru? Ni nani aliyezifungua kamba zake? Nimempa nchi isiyokaliwa na watu kuwa masikani yake, nchi ya chumvi kuwa makao yake. Huzicheka ghasia za mji, wala hasikii kelele za mwendesha gari. Huzunguka vilimani kwa ajili ya malisho na kutafuta kila kitu kibichi. “Je, nyati atakubali kukutumikia? Atakaa karibu na hori lako usiku? Je, unaweza kumfungia kwenye matuta kwa kamba? Je, atalima mabonde nyuma yako? Je, utamtumainia kwa ajili ya nguvu zake nyingi? Utamwachia yeye kazi zako nzito? Utaweza kumwamini akuletee nafaka yako nyumbani kutoka shambani na kuikusanya kwenye sakafu yako ya kupuria?
Yobu 39:1-12 Biblia Habari Njema (BHN)
“Je, wajua mbuzi wa milimani huzaa lini, au umewahi kuona kulungu akizaa? Je, wajua huchukua mimba kwa muda gani, au siku yenyewe ya kuzaa waijua? “Wajua wakati watakapochuchumaa kuzaa, wakati wa kuzaa watoto wao? Watoto wao hupata nguvu, hukua hukohuko porini, kisha huwaacha mama zao na kwenda zao. “Nani aliyemwacha huru pundamwitu? Nani aliyewaacha waende kwa kuwafungua? Mimi niliwapa jangwa liwe makao yao, mbuga zenye chumvi kuwa makazi yao. Hujitenga kabisa na makelele ya miji, hasikilizi kelele ya kumfanyisha kazi. Hutembeatembea milimani kupata malisho, na kutafuta chochote kilicho kibichi. “Je, nyati atakubali kukutumikia? Au je, atakubali kulala zizini mwako? Je, waweza kumfunga nyati kamba kulima shamba, au avute jembe la kulimia? Je, utamtegemea kwa kuwa ana nguvu nyingi na kumwacha akufanyie kazi zako nzito? Je, wamtazamia nyati akuvunie mavuno yako, na kuleta nafaka mahali pa kupuria?

Yobu 39:1-12 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Je! Wajua majira ya kuzaa kwao mbuzi-mwitu walio majabalini? Au waweza kusema majira ya kuzaa kulungu? Je! Waweza kuhesabu miezi yao watakayoitimiza? Au je! Wajua majira ya kuzaa kwao? Wao hujiinamisha, kuzaa watoto wao, Watupa taabu zao. Watoto wao wa katika hali nzuri, hukua katika bara wazi; Huenda zao, wala hawarudi tena. Ni nani aliyempeleka punda-milia aende huru? Au je! Ni nani aliyemfungulia vifungo punda-mwitu? Ambaye nimeifanya nyika kuwa nyumba yake, Na nchi ya chumvi kuwa makao yake. Yeye hudharau mshindo wa mji, Wala hasikii kelele zake msimamizi. Upana wa milima ni malisho yake, Hutafuta-tafuta kila kitu kilicho kibichi. Je! Nyati atakubali kukutumikia? Au atakaa katika zizi lako? Je! Waweza kumfunga nyati kwa kamba matutani? Au, yeye atayalima mabonde nyuma yako? Je! Utamtumaini kwa sababu ana nguvu nyingi? Au, utamwachia yeye kazi yako? Je! Utamtumaini kwamba ataileta mbegu yako nyumbani. Na kukusanya nafaka ya kiwanja chako cha kupuria?