Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Isaya 55:3-11

Isaya 55:3-11 NENO

Tegeni sikio mje kwangu, nisikieni mimi, ili nafsi zenu zipate kuishi. Nitafanya agano la milele nanyi, pendo la uaminifu nililomwahidi Daudi. Tazama, nimemfanya kuwa shahidi wa mataifa, kiongozi na jemadari wa mataifa. Hakika utaita mataifa usiyoyajua, nayo mataifa yale yasiyokujua yataharakisha kukujia, kwa sababu ya Mwenyezi Mungu, Mungu wako, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli, kwa maana amekutukuza.” Mtafuteni Mwenyezi Mungu maadamu anapatikana; mwiteni maadamu yu karibu. Mtu mwovu na aiache njia yake, na mtu mbaya na ayaache mawazo yake. Yeye na amrudie Mwenyezi Mungu, naye atamrehemu, arudi kwa Mungu wetu, kwa kuwa atamsamehe bure kabisa. “Kwa kuwa mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu,” asema Mwenyezi Mungu. “Kama vile mbingu zilivyo juu kuliko dunia, ndivyo njia zangu zilivyo juu kuliko njia zenu na mawazo yangu kuliko mawazo yenu. Kama vile mvua na theluji ishukavyo kutoka mbinguni, nayo hairudi tena huko bila kunywesha dunia na kuichipusha na kuistawisha, ili itoe mbegu kwa mpanzi na mkate kwa mlaji, ndivyo lilivyo neno langu litokalo kinywani mwangu: Halitanirudia tupu, bali litatimiliza lile nililokusudia, na litafanikiwa katika kusudi lile nililolituma.