Isaya 55:3-11
Isaya 55:3-11 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Tegeni masikio yenu, na kunijia; Sikieni, na nafsi zenu zitaishi; Nami nitafanya nanyi agano la milele, Naam, rehema za Daudi zilizo imara. Angalieni, nimemweka kuwa shahidi kwa kabila za watu; kuwa kiongozi na jemadari kwa kabila za watu. Tazama, utaita taifa usilolijua, na taifa lisilokujua wewe litakukimbilia, kwa sababu ya BWANA, Mungu wako, na kwa ajili yake Mtakatifu wa Israeli; maana amekutukuza. Mtafuteni BWANA, maadamu anapatikana, Mwiteni, maadamu yu karibu; Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na amrudie BWANA, Naye atamrehemu; Na arejee kwa Mungu wetu, Naye atamsamehe kabisa. Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema BWANA. Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu. Maana kama vile mvua ishukavyo, na theluji, kutoka mbinguni, wala hairudi huko; bali huinywesha ardhi, na kuizalisha na kuichipuza, ikampa mtu apandaye mbegu, na mtu alaye chakula; ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.
Isaya 55:3-11 Biblia Habari Njema (BHN)
“Tegeni sikio enyi watu wangu, mje kwangu; nisikilizeni, ili mpate kuishi. Nami nitafanya nanyi agano la milele; nitawapeni fadhili nilizomwahidi Daudi. Mimi nilimfanya kiongozi na kamanda wa mataifa ili yeye anishuhudie kwa watu wa mataifa. Sasa utayaita mataifa usiyoyajua, watu wa mataifa yasiyokutambua watakujia mbio, kwa sababu yangu mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako; kwa sababu yangu mimi Mtakatifu wa Israeli niliyekufanya wewe utukuke.” Mtafuteni Mwenyezi-Mungu wakati bado anapatikana, mwombeni msaada wakati yupo bado karibu. Waovu na waache njia zao mbaya, watu wabaya waachane na mawazo yao mabaya; wamrudie Mwenyezi-Mungu apate kuwahurumia, wamwendee Mungu wetu maana atawasamehe. Maana, Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Mawazo yangu si kama mawazo yenu, wala njia zangu si kama njia zenu. Kama vile mbingu zilivyo mbali na dunia, ndivyo njia zangu zilivyo mbali na zenu, na mawazo yangu mbali na mawazo yenu. “Kama vile mvua na theluji ishukavyo toka mbinguni, wala hairudi huko bali huinywesha ardhi, ikaifanya ichipue mimea ikakua, ikampatia mpanzi mbegu na kuwapa watu chakula, vivyo hivyo na neno langu mimi: Halitanirudia bila mafanikio, bali litatekeleza matakwa yangu, litafanikiwa lengo nililoliwekea.
Isaya 55:3-11 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Tegeni masikio yenu, na kunijia; Sikieni, na nafsi zenu zitaishi; Nami nitafanya nanyi agano la milele, Naam, rehema za Daudi zilizo imara. Angalieni, nimemweka kuwa shahidi kwa makabila ya watu; kuwa kiongozi na jemadari kwa makabila ya watu. Tazama, utaita taifa usilolijua, na taifa lisilokujua wewe litakukimbilia, kwa sababu ya BWANA, Mungu wako, na kwa ajili yake Mtakatifu wa Israeli; maana amekutukuza. Mtafuteni BWANA, maadamu anapatikana, Mwiteni, maadamu yuko karibu; Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na amrudie BWANA, Naye atamrehemu; Na arejee kwa Mungu wetu, Naye atamsamehe kabisa. Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema BWANA. Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, ndivyo njia zangu zilivyo juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu. Maana kama vile mvua ishukavyo, na theluji, kutoka mbinguni, wala hairudi huko; bali huinywesha ardhi, na kuizalisha na kuichipuza, ikampa mtu apandaye mbegu, na mtu alaye chakula; ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.
Isaya 55:3-11 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Tegeni masikio yenu, na kunijia; Sikieni, na nafsi zenu zitaishi; Nami nitafanya nanyi agano la milele, Naam, rehema za Daudi zilizo imara. Angalieni, nimemweka kuwa shahidi kwa kabila za watu; kuwa kiongozi na jemadari kwa kabila za watu. Tazama, utaita taifa usilolijua, na taifa lisilokujua wewe litakukimbilia, kwa sababu ya BWANA, Mungu wako, na kwa ajili yake Mtakatifu wa Israeli; maana amekutukuza. Mtafuteni BWANA, maadamu anapatikana, Mwiteni, maadamu yu karibu; Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na amrudie BWANA, Naye atamrehemu; Na arejee kwa Mungu wetu, Naye atamsamehe kabisa. Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema BWANA. Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu. Maana kama vile mvua ishukavyo, na theluji, kutoka mbinguni, wala hairudi huko; bali huinywesha ardhi, na kuizalisha na kuichipuza, ikampa mtu apandaye mbegu, na mtu alaye chakula; ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.
Isaya 55:3-11 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Tegeni sikio mje kwangu, nisikieni mimi, ili nafsi zenu zipate kuishi. Nitafanya agano la milele nanyi, pendo la uaminifu nililomwahidi Daudi. Tazama, nimemfanya kuwa shahidi wa mataifa, kiongozi na jemadari wa mataifa. Hakika utaita mataifa usiyoyajua, nayo mataifa yale yasiyokujua yataharakisha kukujia, kwa sababu ya BWANA Mungu wako, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli, kwa maana amekutukuza.” Mtafuteni BWANA maadamu anapatikana; mwiteni maadamu yu karibu. Mtu mwovu na aiache njia yake, na mtu mbaya na ayaache mawazo yake. Yeye na amrudie BWANA, naye atamrehemu, arudi kwa Mungu wetu, kwa kuwa atamsamehe bure kabisa. “Kwa kuwa mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu,” asema BWANA. “Kama vile mbingu zilivyo juu kuliko dunia, ndivyo njia zangu zilivyo juu kuliko njia zenu na mawazo yangu kuliko mawazo yenu. Kama vile mvua na theluji ishukavyo kutoka mbinguni, nayo hairudi tena huko bila kunywesha dunia na kuichipusha na kuistawisha, hivyo hutoa mbegu kwa mpanzi na mkate kwa mlaji, ndivyo lilivyo neno langu lile litokalo kinywani mwangu: Halitanirudia tupu, bali litatimiliza lile nililokusudia na litafanikiwa katika kusudi lile nililolituma.