Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Isaya 14:24-32

Isaya 14:24-32 NENO

Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni ameapa, “Hakika, kama vile nilivyopanga, ndivyo itakavyokuwa, nami kama nilivyokusudia, ndivyo itakavyosimama. Nitamponda Mwashuru katika nchi yangu, juu ya milima yangu nitawakanyagia chini. Nira yake itaondolewa kutoka kwa watu wangu, nao mzigo wake utaondolewa kutoka mabegani mwao.” Huu ndio mpango uliokusudiwa kwa ajili ya ulimwengu wote, huu ni mkono ulionyooshwa juu ya mataifa yote. Kwa kuwa Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni amekusudia, ni nani awezaye kumzuia? Mkono wake umenyooshwa, ni nani awezaye kuurudisha? Neno hili lilikuja mwaka ule Mfalme Ahazi alipofariki: Msifurahi, enyi Wafilisti wote, kwamba fimbo iliyowapiga imevunjika; kutoka mzizi wa huyo nyoka atachipuka nyoka mwenye sumu kali, uzao wake utakuwa joka lirukalo, lenye sumu kali. Maskini kuliko maskini wote watapata malisho, nao wahitaji watalala salama. Lakini mzizi wako nitauangamiza kwa njaa, nayo njaa itawaua walionusurika. Piga yowe, ee lango! Bweka, ee mji! Yeyukeni, enyi Wafilisti wote! Wingu la moshi linakuja toka kaskazini, wala hakuna atakayechelewa katika safu zake. Ni jibu gani litakalotolewa kwa wajumbe wa taifa hilo? “Mwenyezi Mungu ameifanya imara Sayuni, na ndani yake watu wake walioonewa watapata kimbilio.”