Isaya 14:24-32
Isaya 14:24-32 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni ameapa, “Hakika, kama vile nilivyopanga, ndivyo itakavyokuwa, nami kama nilivyokusudia, ndivyo itakavyosimama. Nitamponda Mwashuru katika nchi yangu, juu ya milima yangu nitawakanyagia chini. Nira yake itaondolewa kutoka kwa watu wangu, nao mzigo wake utaondolewa kutoka mabegani mwao.” Huu ndio mpango uliokusudiwa kwa ajili ya ulimwengu wote, huu ni mkono ulionyooshwa juu ya mataifa yote. Kwa kuwa Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni amekusudia, ni nani awezaye kumzuia? Mkono wake umenyooshwa, ni nani awezaye kuurudisha? Neno hili lilikuja mwaka ule Mfalme Ahazi alipofariki: Msifurahi, enyi Wafilisti wote, kwamba fimbo iliyowapiga imevunjika; kutoka mzizi wa huyo nyoka atachipuka nyoka mwenye sumu kali, uzao wake utakuwa joka lirukalo, lenye sumu kali. Maskini kuliko maskini wote watapata malisho, nao wahitaji watalala salama. Lakini mzizi wako nitauangamiza kwa njaa, nayo njaa itawaua walionusurika. Piga yowe, ee lango! Bweka, ee mji! Yeyukeni, enyi Wafilisti wote! Wingu la moshi linakuja toka kaskazini, wala hakuna atakayechelewa katika safu zake. Ni jibu gani litakalotolewa kwa wajumbe wa taifa hilo? “Mwenyezi Mungu ameifanya imara Sayuni, na ndani yake watu wake walioonewa watapata kimbilio.”
Isaya 14:24-32 Swahili Revised Union Version (SRUV)
BWANA wa majeshi ameapa, akisema, Hakika yangu kama vile vilivyoazimia, ndivyo itakavyokuwa; na kama nilivyokusudia, ndivyo itakavyotokea; kwamba nitamvunja huyo Mwashuri vipande vipande katika nchi yangu, na juu ya mlima wangu nitamkanyaga chini ya miguu yangu; ndipo nira yake iliyo juu yao itakapoondoka, na mzigo wake utatoka mabegani mwao. Hilo ndilo kusudi lililokusudiwa duniani kote, na huo ndio mkono ulionyoshwa juu ya mataifa yote. Maana BWANA wa majeshi amekusudia, naye ni nani atakayelibatili? Na mkono wake ulionyoshwa, ni nani atakayeugeuza nyuma? Ufunuo huu ulikuja mwaka ule alipokufa mfalme Ahazi. Msifurahi, Enyi Wafilisti wote, Kwa sababu fimbo ile iliyokupiga imevunjika; Maana katika shina la nyoka atatoka fira, Na uzao wake ni joka la moto arukaye Sef 2:4-7; Zek 9:5-7 Nao walio maskini kabisa watakula, Na wahitaji watajilaza salama; Nami nitatia shina lako kwa njaa, Na mabaki yako watauawa. Piga yowe, Ee lango; lia, Ee mji; Ee Ufilisti enyi wote, umeyeyuka kabisa; Maana moshi unakuja toka kaskazini, Wala hakuna atakayechelewa katika majeshi yake. Wajumbe wa taifa hilo waletewe jibu gani? Ya kuwa BWANA ameiweka misingi ya Sayuni, na ndani yake wale walioonewa katika watu wake watapata kimbilio kwake.
Isaya 14:24-32 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu wa majeshi ameapa: “Kama nilivyopanga, ndivyo itakavyokuwa; kama nilivyokusudia, ndivyo itakavyokamilika. Nitauvunja uwezo wa Waashuru nchini mwangu; nitawakanyagakanyaga katika milima yangu. Nitawaondolea watu wangu nira ya dhuluma yao, na mzigo wa mateso yao.” Huu ndio uamuzi wake Mwenyezi-Mungu kuhusu dunia yote; hii ndiyo adhabu atakayotoa juu ya mataifa yote. Kama Mwenyezi-Mungu wa majeshi ameamua, nani atakayeweza kubatilisha uamuzi wake? Kama amepania kutoa adhabu, ni nani atakayempinga? Mwaka alipofariki mfalme Ahazi, Mungu alitoa kauli hii: “Msishangilie enyi Wafilisti wote, kwamba Ashuru, fimbo iliyowapiga, imevunjika; maana, nyoka wa kawaida atazaa nyoka mwenye sumu, na nyoka mwenye sumu atazaa joka lirukalo. Wazaliwa wa kwanza wa maskini watashiba, na fukara watakaa kwa usalama. Lakini chipukizi wenu nitawaua kwa njaa; na yeyote wenu atakayebaki nitamuua. Piga yowe ewe lango; lia ewe mji; yeyuka kwa hofu ewe nchi yote ya Filistia. Maana moshi wa askari waja kutoka kaskazini, wala hakuna atakayechelewa katika majeshi yake.” Basi watapewa jibu gani wajumbe wa taifa hilo? Wataambiwa: Mwenyezi-Mungu ameijenga imara Siyoni, na maskini wa watu wake watakimbilia usalama huko.
Isaya 14:24-32 Swahili Revised Union Version (SRUV)
BWANA wa majeshi ameapa, akisema, Hakika yangu kama vile vilivyoazimia, ndivyo itakavyokuwa; na kama nilivyokusudia, ndivyo itakavyotokea; kwamba nitamvunja huyo Mwashuri vipande vipande katika nchi yangu, na juu ya mlima wangu nitamkanyaga chini ya miguu yangu; ndipo nira yake iliyo juu yao itakapoondoka, na mzigo wake utatoka mabegani mwao. Hilo ndilo kusudi lililokusudiwa duniani kote, na huo ndio mkono ulionyoshwa juu ya mataifa yote. Maana BWANA wa majeshi amekusudia, naye ni nani atakayelibatili? Na mkono wake ulionyoshwa, ni nani atakayeugeuza nyuma? Ufunuo huu ulikuja mwaka ule alipokufa mfalme Ahazi. Msifurahi, Enyi Wafilisti wote, Kwa sababu fimbo ile iliyokupiga imevunjika; Maana katika shina la nyoka atatoka fira, Na uzao wake ni joka la moto arukaye Sef 2:4-7; Zek 9:5-7 Nao walio maskini kabisa watakula, Na wahitaji watajilaza salama; Nami nitatia shina lako kwa njaa, Na mabaki yako watauawa. Piga yowe, Ee lango; lia, Ee mji; Ee Ufilisti enyi wote, umeyeyuka kabisa; Maana moshi unakuja toka kaskazini, Wala hakuna atakayechelewa katika majeshi yake. Wajumbe wa taifa hilo waletewe jibu gani? Ya kuwa BWANA ameiweka misingi ya Sayuni, na ndani yake wale walioonewa katika watu wake watapata kimbilio kwake.
Isaya 14:24-32 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
BWANA wa majeshi ameapa, akisema, Hakika yangu kama vile vilivyoazimia, ndivyo itakavyokuwa; na kama nilivyokusudia, ndivyo itakavyotokea; kwamba nitamvunja huyo Mwashuri vipande vipande katika nchi yangu, na juu ya mlima wangu nitamkanyaga chini ya miguu yangu; ndipo nira yake iliyo juu yao itakapoondoka, na mzigo wake utatoka mabegani mwao. Hilo ndilo kusudi lililokusudiwa duniani mwote, na huo ndio mkono ulionyoshwa juu ya mataifa yote. Maana BWANA wa majeshi amekusudia, naye ni nani atakayelibatili? Na mkono wake ulionyoshwa, ni nani atakayeugeuza nyuma? Ufunuo huu ulikuja mwaka ule alipokufa mfalme Ahazi. Usifurahi, Ee Ufilisti, pia wote, Kwa sababu fimbo ile iliyokupiga imevunjika; Maana katika shina la nyoka atatoka fira, Na uzao wake ni joka la moto arukaye Sef 2:4-7; Zek 9:5-7 Nao walio maskini kabisa watakula, Na wahitaji watajilaza salama; Nami nitatia shina lako kwa njaa, Na mabaki yako watauawa. Piga yowe, Ee lango; lia, Ee mji; Ee Ufilisti, pia wote, umeyeyuka kabisa; Maana moshi unakuja toka kaskazini, Wala hakuna atakayechelewa katika majeshi yake. Wajumbe wa taifa hilo waletewe jibu gani? Ya kuwa BWANA ameiweka misingi ya Sayuni, na ndani yake wale walioonewa katika watu wake wataona kimbilio.