Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Waebrania 7:18-25

Waebrania 7:18-25 NENO

Kwa upande mmoja, ile amri ya mwanzo isiyofaa na dhaifu imebatilishwa (kwa maana sheria haikufanya kitu chochote kuwa kikamilifu). Kwa upande mwingine, tumeletewa tumaini lililo bora zaidi ambalo linatuleta karibu na Mungu. Nalo tumaini hilo halikutolewa pasipo kiapo! Wengine walikuwa makuhani pasipo kiapo chochote, lakini Isa alifanywa kuhani kwa kiapo wakati Mungu alimwambia: “Mwenyezi Mungu ameapa, naye hatabadilisha mawazo yake: ‘Wewe ni kuhani milele.’” Kwa ajili ya kiapo hiki, Isa amekuwa mdhamini wa agano lililo bora zaidi. Basi kumekuwa na makuhani wengi wa aina hiyo, kwa kuwa kifo kiliwazuia kuendelea na huduma yao ya ukuhani. Lakini kwa sababu Isa anaishi milele, anao ukuhani wa kudumu. Kwa hiyo anaweza kuwaokoa kabisa wale wanaomjia Mungu kupitia kwake, kwa sababu yeye adumu daima kuomba kwa ajili yao.