Waebrania 7:18-25
Waebrania 7:18-25 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Maana, kuna kubatiliwa kwa ile amri iliyotangulia, kwa sababu ya udhaifu wake, na kutokufaa kwake; (kwa maana ile sheria haikukamilisha neno); na pamoja na hayo kuliingizwa matumaini yaliyo mazuri zaidi, ambayo kwa hayo tunamkaribia Mungu. Na kwa kuwa haikuwa pasipo kiapo, (maana wale walifanywa makuhani pasipo kiapo; bali yeye, pamoja na kiapo, kwa yeye aliyemwambia, Bwana ameapa wala hataghairi, Wewe u kuhani milele;) basi kwa kadiri hii Yesu amekuwa mdhamini wa agano lililo bora zaidi. Tena wale walifanywa makuhani wengi, kwa sababu walizuiliwa na mauti wasikae; bali yeye, kwa kuwa anakaa milele, anao ukuhani wake usioondoka. Naye, kwa sababu hii, anaweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee.
Waebrania 7:18-25 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Kwa upande mmoja, ile amri ya mwanzo isiyofaa na dhaifu imebatilishwa (kwa maana sheria haikufanya kitu chochote kuwa kikamilifu). Kwa upande mwingine, tumeletewa tumaini lililo bora zaidi ambalo linatuleta karibu na Mungu. Nalo tumaini hilo halikutolewa pasipo kiapo! Wengine walikuwa makuhani pasipo kiapo chochote, lakini Isa alifanywa kuhani kwa kiapo wakati Mungu alimwambia: “Mwenyezi Mungu ameapa, naye hatabadilisha mawazo yake: ‘Wewe ni kuhani milele.’” Kwa ajili ya kiapo hiki, Isa amekuwa mdhamini wa agano lililo bora zaidi. Basi kumekuwa na makuhani wengi wa aina hiyo, kwa kuwa kifo kiliwazuia kuendelea na huduma yao ya ukuhani. Lakini kwa sababu Isa anaishi milele, anao ukuhani wa kudumu. Kwa hiyo anaweza kuwaokoa kabisa wale wanaomjia Mungu kupitia kwake, kwa sababu yeye adumu daima kuomba kwa ajili yao.
Waebrania 7:18-25 Biblia Habari Njema (BHN)
Basi, ile amri ya zamani ilifutwa kwa sababu ilikuwa hafifu na isiyofaa kitu. Maana sheria ya Mose haikuweza kukamilisha jambo lolote. Lakini sasa, mahali pake pamewekwa tumaini lililo bora zaidi ambalo kwalo tunaweza kumkaribia Mungu. Zaidi ya hayo, hapa pana kiapo cha Mungu. Wakati wale wengine walipofanywa makuhani hapakuwako kiapo. Lakini Yesu alifanywa kuhani kwa kiapo wakati Mungu alipomwambia: “Bwana ameapa, wala hatabadili nia yake: ‘Wewe ni kuhani milele.’” Basi, kutokana na tofauti hii, Yesu amekuwa mdhamini wa agano lililo bora zaidi. Tena: Hao makuhani wengine walikuwa wengi kwa sababu walikufa na hawakuweza kuendelea na kazi yao. Lakini Yesu si kama wao, yeye anaishi milele; ukuhani wake hauondoki kwake. Hivyo, yeye anaweza daima kuwaokoa kabisa wote wanaomwendea Mungu kwa njia yake, maana yeye anaishi milele kuwaombea kwa Mungu.
Waebrania 7:18-25 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Maana, kuna kubatiliwa kwa ile amri iliyotangulia, kwa sababu ya udhaifu wake, na kutokufaa kwake; (kwa maana ile sheria haikukamilisha neno); na pamoja na hayo kuliingizwa matumaini yaliyo mazuri zaidi, ambayo kwa hayo tunamkaribia Mungu. Na kwa kuwa haikuwa pasipo kiapo, (maana wale walifanywa makuhani pasipo kiapo; bali yeye, pamoja na kiapo, kwa yeye aliyemwambia, Bwana ameapa wala hataghairi, Wewe u kuhani milele;) basi kwa kadiri hii Yesu amekuwa mdhamini wa agano lililo bora zaidi. Tena wale walifanywa makuhani wengi, kwa sababu walizuiliwa na mauti wasikae; bali yeye, kwa kuwa anakaa milele, anao ukuhani wake usioondoka. Naye, kwa sababu hii, anaweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee.
Waebrania 7:18-25 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Maana, kuna kubatiliwa kwa ile amri iliyotangulia, kwa sababu ya udhaifu wake, na kutokufaa kwake; (kwa maana ile sheria haikukamilisha neno); na pamoja na hayo kuliingizwa matumaini yaliyo mazuri zaidi, ambayo kwa hayo twamkaribia Mungu. Na kwa kuwa haikuwa pasipo kiapo, (maana wale walifanywa makuhani pasipo kiapo; bali yeye, pamoja na kiapo, kwa yeye aliyemwambia, Bwana ameapa wala hataghairi, Wewe u kuhani milele;) basi kwa kadiri hii Yesu amekuwa mdhamini wa agano lililo bora zaidi. Tena wale walifanywa makuhani wengi, kwa sababu wazuiliwa na mauti wasikae; bali yeye, kwa kuwa akaa milele, anao ukuhani wake usioondoka. Naye, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee.