Mhubiri Utangulizi
Utangulizi
Neno “Mhubiri” linatokana na neno la Kiebrania “Qoheleth” ambalo linamaanisha “Anayehutubia kusanyiko la watu”, na linatafsiriwa kama “Mwalimu” katika “Septuaginta”. Mara kwa mara mwandishi wa kitabu hiki anajitambulisha mwenyewe kuwa “Mhubiri”. Neno hili limetumiwa mara saba katika kitabu hiki. Hivyo, ilionekana inafaa kutumia neno hili kukitambulisha kitabu hiki.
Mwandishi
Inadhaniwa kuwa ni Sulemani.
Kusudi
Kuchunguza kwa kina maana ya maisha kwa ujumla, na kuonesha kuwa maisha hayana maana, yaani ni ubatili, kama hakuna kumcha Mungu kikamilifu.
Mahali
Yerusalemu.
Tarehe
Inadhaniwa kuwa mwaka 935 K.K., mwishoni mwa maisha ya Sulemani.
Wahusika Wakuu
Sulemani.
Wazo Kuu
Ili kuelewa maisha na kufanya uamuzi ulio sawa, binadamu anahitaji hekima ambayo inapatikana kwa kumjua Mungu pekee.
Mambo Muhimu
Kuonesha jinsi kufuata starehe maishani kunaweza kuleta udanganyifu wa dhambi na kutukosesha utoshelevu na furaha. Chanzo cha furaha, mafanikio na utoshelevu ni kumcha Mungu na kuzishika amri zake. Kama mtu yeyote ataishi na Mungu daima, basi kumtii Mungu ndio njia pekee ya kufanikiwa katika maisha ya hapa duniani.
Yaliyomo
Maisha ni ubatili mtupu (1:1‑11)
Kikomo cha hekima (1:12–2:26)
Kila jambo lina wakati wake (3:1‑22)
Ugumu wa maisha na kumcha Mungu (4:1–6:12)
Hekima na kutosheka (7:1–8:17)
Maisha ni lazima yatawaliwe na hekima (9:1–11:6)
Hekima ya kweli ni kumcha Mungu (11:7–12:14).
Iliyochaguliwa sasa
Mhubiri Utangulizi: NENO
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Neno: Biblia Takatifu™ Neno™
Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 na Biblica, Inc.
Imetumiwa kwa ruhusa. Haki zote zimehifadhiwa duniani kote.
Kiswahili Contemporary Version™
Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 by Biblica, Inc.
Used with permission. All rights reserved worldwide.