Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mhubiri Utangulizi

Utangulizi
Neno “Mhubiri” linatokana na neno la Kiebrania “Qoheleth” ambalo linamaanisha “Anayehutubia kusanyiko la watu”, na linatafsiriwa kama “Mwalimu” katika “Septuaginta”. Mara kwa mara mwandishi wa kitabu hiki anajitambulisha mwenyewe kuwa “Mhubiri”. Neno hili limetumiwa mara saba katika kitabu hiki. Hivyo, ilionekana inafaa kutumia neno hili kukitambulisha kitabu hiki.
Mwandishi
Inadhaniwa kuwa ni Sulemani.
Kusudi
Kuchunguza kwa kina maana ya maisha kwa ujumla, na kuonesha kuwa maisha hayana maana, yaani ni ubatili, kama hakuna kumcha Mwenyezi Mungu kikamilifu.
Mahali
Yerusalemu.
Tarehe
Inadhaniwa kuwa mwaka 935 K.K., mwishoni mwa maisha ya Sulemani.
Wahusika Wakuu
Sulemani.
Wazo Kuu
Ili kuelewa maisha na kufanya uamuzi ulio sawa, binadamu anahitaji hekima ambayo inapatikana kwa kumjua Mwenyezi Mungu pekee.
Mambo Muhimu
Kuonesha jinsi kufuata starehe maishani kunaweza kuleta udanganyifu wa dhambi na kutukosesha utoshelevu na furaha. Chanzo cha furaha, mafanikio na utoshelevu ni kumcha Mwenyezi Mungu na kuzishika amri zake. Kama mtu yeyote ataishi na Mwenyezi Mungu daima, basi kumtii Mwenyezi Mungu ndio njia pekee ya kufanikiwa katika maisha ya hapa duniani.
Yaliyomo
Maisha ni ubatili mtupu (1:1-11)
Kikomo cha hekima (1:12–2:26)
Kila jambo lina wakati wake (3:1-22)
Ugumu wa maisha na kumcha Mwenyezi Mungu (4:1–6:12)
Hekima na kutosheka (7:1–8:17)
Maisha ni lazima yatawaliwe na hekima (9:1–11:6)
Hekima ya kweli ni kumcha Mwenyezi Mungu (11:7–12:14).

Iliyochaguliwa sasa

Mhubiri Utangulizi: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia