Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kumbukumbu Utangulizi

Utangulizi
Kitabu hiki ndicho cha mwisho katika ule mgawanyo wa kwanza wa Maandiko Matakatifu ambao huitwa “Torati.” Katika hotuba zilizonakiliwa katika Kumbukumbu la Torati, Musa anafanya ufupisho wa dini ya Wayahudi kuwa Agano lililotolewa kwa baba zao. Hili Agano ndilo msingi wa uhusiano ulioanzishwa na Mwenyezi Mungu baina yake na Waisraeli, wala si Torati, ambayo sasa inadhihirishwa kwa Waisraeli kwa kuokolewa kutoka Misri na kutunzwa kwa muda wote wa kutangatanga huko jangwani. Baada ya miaka arobaini, Waisraeli walikuwa wamekaribia kuingia katika Nchi ya Ahadi. Lakini kabla ya kufanya hivyo, Musa alitaka kuwakumbusha historia yao, yaani yale yote ambayo Mwenyezi Mungu alikuwa amewatendea, pamoja na amri zile zote walizopaswa kuendelea kutii kama taifa teule la Mwenyezi Mungu.
Mazungumzo ya kwanza ya Musa yalikuwa kuwakumbusha watu kuhusu wema wa Mwenyezi Mungu kwa kipindi chote cha safari ili kuwapa nchi ya Kanaani. Mazungumzo ya pili yalikuwa ni muhtasari wa Sheria za Mwenyezi Mungu zikiwepo Amri Kumi. Musa aliwaambia watu, “Mpende Mwenyezi Mungu, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote” (6:5) ili waweze kuendelea kuzifurahia baraka za Mwenyezi Mungu. Pia Musa alitilia mkazo ukweli kwamba ili waweze kuwa na uhusiano mzuri na Mwenyezi Mungu, ilikuwa ni lazima watu wawafundishe watoto wao kumpenda Mwenyezi Mungu na kuzitii amri zake. Kutokana na hilo, haki na uadilifu zingepenya katika maisha yao ya kila siku, kadiri ambavyo upendo wao ungeelekezwa kwa ndugu wa kiume na wa kike.
Mwandishi
Musa, isipokuwa sura inayoeleza kuhusu kifo chake.
Kusudi
Kuwakumbusha Waisraeli kuhusu mambo yale Mwenyezi Mungu alikuwa amewatendea, na kuwahimiza wajitoe kabisa kwake.
Mahali
Mashariki mwa Mto Yordani, karibu na Yeriko, wakiwa wanaikabili nchi ya Kanaani.
Tarehe
Mnamo 1407–1406 K.K.
Wahusika Wakuu
Musa, Yoshua, na Waisraeli.
Wazo Kuu
Kitabu cha Kumbukumbu la Torati kinaishia kwa kuwakumbusha Waisraeli juu ya Agano ambalo Mwenyezi Mungu alifanya nao (29), kuteuliwa kwa Yoshua kuwa kiongozi mpya (31), na kifo cha Musa (34).
Mambo Muhimu
Ili kudumisha uhusiano wa upendo kati ya Waisraeli na Mwenyezi Mungu, wazazi waliagizwa kuwafundisha watoto wao kumcha Mwenyezi Mungu kwa kuwafundisha kwa kielelezo (4:9-10; 6:7). Kwa kuadhimisha zile sikukuu za mwaka, yaani Pasaka, Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, Sikukuu ya Majuma, Sikukuu ya Vibanda, Sikukuu ya Mavuno, pamoja na yale makusanyiko mengine, Waisraeli walivikumbusha vizazi vilivyofuata juu ya upendo wa Mwenyezi Mungu uliooneshwa kwenye ukombozi wao kutolewa Misri na kuendelea kwao kutunzwa naye kwa kuwapa mazao.
Yaliyomo
Utangulizi na mazungumzo ya kwanza ya Musa (1:1–4:43)
Mazungumzo ya pili ya Musa (4:44–11:32)
Sheria za maisha ya kila siku (12:1–26:19)
Matokeo ya kutii na ya kutokutii (27:1–28:68)
Kufanya upya agano (29:1–30:20)
Baraka za Musa kwa Israeli, na kifo cha Musa (31:1–34:12).

Iliyochaguliwa sasa

Kumbukumbu Utangulizi: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia