Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Hesabu 36

36
Urithi wa binti za Selofehadi
1Viongozi wa jamaa ya ukoo wa Gileadi mwana wa Makiri, mwana wa Manase, waliokuwa wametoka katika koo za wazao wa Yusufu, walikuja na kuzungumza mbele ya Musa na viongozi, wakuu wa jamaa ya Waisraeli. 2Wakasema, “Mwenyezi Mungu alipomwamuru bwana wangu kuwapa Waisraeli nchi kama urithi kwa kura, alikuamuru kutoa urithi wa ndugu yetu Selofehadi kwa binti zake. 3Sasa ikiwa wataolewa na wanaume wa makabila mengine ya Israeli, itakuwa kwamba urithi wao utaondolewa kutoka urithi wa mababu zetu na kuongezwa katika urithi wa kabila ambalo dada hao wameolewa. Kwa hiyo sehemu ya urithi tuliyogawiwa itachukuliwa kutoka kwetu. 4Mwaka wa Yubile kwa Waisraeli utakapofika, urithi wao utaongezwa kwa lile kabila ambalo wameolewa, na mali yao itaondolewa kutoka urithi wa kabila la mababu zetu.”
5Ndipo kwa agizo la Mwenyezi Mungu Musa akatoa amri ifuatayo kwa Waisraeli: “Kile wazao wa kabila la Yusufu wanachosema ni kweli. 6Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu anavyoamuru kwa binti za Selofehadi: Wanaweza kuolewa na mtu yeyote wampendaye, mradi tu waolewe miongoni mwa koo za kabila la baba yao. 7Hakuna urithi katika Israeli utakaohamishwa kutoka kabila moja kwenda kabila jingine, kwa kuwa kila Mwisraeli atatunza ardhi ya kabila lake aliyoirithi kutoka kwa baba zake. 8Kila binti atakayerithi ardhi katika kabila lolote la Israeli ni lazima aolewe na mtu kutoka kabila na ukoo wa baba yake, ili kila Mwisraeli amiliki urithi wa baba zake. 9Hakuna urithi uwezao kuhamishwa kutoka kabila moja kwenda kabila jingine, kwa kuwa kila kabila la Israeli litatunza nchi linayorithi.”
10Kwa hiyo binti za Selofehadi wakafanya kama Mwenyezi Mungu alivyomwamuru Musa. 11Binti za Selofehadi, ambao ni Mahla, Tirsa, Hogla, Milka na Noa, wakaolewa na wana wa ndugu za baba yao. 12Waliolewa ndani ya koo za wazao wa Manase mwana wa Yusufu, na urithi wao ukabaki katika ukoo na kabila la baba yao.
13Haya ndio maagizo na masharti ambayo Mwenyezi Mungu aliwapa Waisraeli kupitia Musa katika tambarare za Moabu, karibu na Yordani ng’ambo ya Yeriko.

Iliyochaguliwa sasa

Hesabu 36: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia