Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kumbukumbu 8:2-6

Kumbukumbu 8:2-6 NEN

Kumbuka jinsi BWANA Mungu wenu alivyowaongoza katika njia yote katika jangwa kwa miaka hii arobaini, kukunyenyekeza na kukujaribu ili ajue lililoko moyoni mwako, kwamba utayashika maagizo yake au la. Alikudhili na kukufanya uone njaa kisha akulishe kwa mana, ambayo wewe wala baba zako hamkuijua, awafundishe kuwa mwanadamu hataishi kwa mkate tu bali kwa kila neno litokalo katika kinywa cha BWANA. Nguo zenu hazikuchakaa wala miguu yenu haikuvimba kwa miaka hii arobaini. Mjue basi ndani ya mioyo yenu kama mtu anavyomwadibisha mwanawe, ndivyo BWANA Mungu wako atawaadibisha ninyi. Shikeni maagizo ya BWANA Mungu wenu mtembee katika njia zake na kumheshimu.

Video for Kumbukumbu 8:2-6