Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kumbukumbu 23:21-23

Kumbukumbu 23:21-23 NENO

Ukiweka nadhiri kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wako, usichelewe kuitimiza, kwa kuwa Mwenyezi Mungu, Mungu wako, atakudai, nawe utakuwa na hatia ya dhambi. Lakini ukijizuia kuweka nadhiri, hutakuwa na hatia. Chochote kitakachotamkwa kwa midomo yako ni lazima uhakikishe umekifanya, kwa sababu uliweka nadhiri yako kwa hiari mbele za Mwenyezi Mungu, Mungu wako, kwa kinywa chako mwenyewe.