Kumbukumbu la Sheria 23:21-23
Kumbukumbu la Sheria 23:21-23 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Ukiweka nadhiri kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wako, usichelewe kuitimiza, kwa kuwa Mwenyezi Mungu, Mungu wako, atakudai, nawe utakuwa na hatia ya dhambi. Lakini ukijizuia kuweka nadhiri, hutakuwa na hatia. Chochote kitakachotamkwa kwa midomo yako ni lazima uhakikishe umekifanya, kwa sababu uliweka nadhiri yako kwa hiari mbele za Mwenyezi Mungu, Mungu wako, kwa kinywa chako mwenyewe.
Kumbukumbu la Sheria 23:21-23 Biblia Habari Njema (BHN)
Unapoweka nadhiri kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, usichelewe kuitekeleza, maana Mwenyezi-Mungu, Mungu wako ataidai kwako, nawe utakuwa na kosa. Lakini ukiacha kuweka nadhiri hutakuwa na dhambi. Uwe mwangalifu kutimiza nadhiri uliyotamka kwa mdomo wako, maana ulimwahidi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, kwa hiari yako.
Kumbukumbu la Sheria 23:21-23 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Utakapoweka nadhiri kwa BWANA, Mungu wako, usiwe mlegevu katika kuiondoa; kwa kuwa BWANA, Mungu wako, hataacha kuitaka kwako; nayo hivi itakuwa dhambi kwako. Lakini ukijizuia usiweke nadhiri, haitakuwa dhambi kwako. Yaliyotoka midomoni mwako yashike kuyafanya; kwa mfano wa ulivyomwekea nadhiri BWANA, Mungu wako, ni sadaka ya hiari uliyoahidi kwa kinywa chako.
Kumbukumbu la Sheria 23:21-23 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)