Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kumbukumbu 17:8-13

Kumbukumbu 17:8-13 NENO

Kama mashauri yanaletwa katika mahakama zenu ambayo ni magumu zaidi kwenu kuyaamua, ikiwa ni umwagaji wa damu, madai au mashambulio, yapelekeni mahali Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, atakapopachagua. Nendeni kwa makuhani, ambao ni Walawi, na kwa mwamuzi ambaye atakuwa kazini wakati huo. Ulizeni kwao nao watawapa maamuzi. Ni lazima mtende sawasawa na maamuzi watakayowapa mahali Mwenyezi Mungu atakapopachagua. Kuweni waangalifu kufanya kila kitu watakachowaongoza kufanya. Fanyeni sawasawa na sheria wanayowafundisha na maamuzi wanayowapa. Msigeuke mkono wa kuume au kushoto kuacha kufanya yale wanayowaambia. Mwanaume atakayeonesha dharau kwa mwamuzi au kwa kuhani ambaye amewekwa kumtumikia Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, lazima auawe. Lazima mwondoe uovu katika Israeli. Watu wote watasikia na kuogopa, nao hawatakuwa wenye kudharau tena.