Kumbukumbu la Sheria 17:8-13
Kumbukumbu la Sheria 17:8-13 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ikiwa limezuka neno lililo zito kukupita wewe, katika maamuzi kati ya damu na damu, na kati ya kesi na kesi, na kati ya pigo na pigo, nayo yashindaniwa katika malango yako; ndipo nawe uondoke, ukwee uende mahali atakapochagua BWANA, Mungu wako; uwaendee makuhani Walawi, na mwamuzi atakayekuwako siku hizo; uwaulize; nao watakuonesha hukumu ya maamuzi; nawe fanya sawasawa na hukumu watakayokuonesha mahali hapo atakapochagua BWANA; nawe tunza kufanya kwa mfano wa yote watakayokufunza; kwa mfano wa sheria watakayokufunza, na kwa mfano wa hukumu watakayokuambia, fanya vivyo hivyo; usigeuke katika hukumu watakayokuonesha, kwenda mkono wa kulia wala wa kushoto. Na mtu afanyaye kwa kujikinai, kwa kutomsikiza kuhani asimamaye hapo kwa kumtumikia BWANA, Mungu wako, au mwamuzi, na afe mtu huyo; nawe utauondoa uovu katika Israeli. Na hao watu wote watasikia na kuogopa, wasifanye tena kwa kujikinai.
Kumbukumbu la Sheria 17:8-13 Biblia Habari Njema (BHN)
Inawezekana kukatokea mashtaka mengine yaliyo magumu mijini mwenu, kama vile kesi zihusuzo: Unajisi, mambo ya haki za watu, na madhara ya mwili. Ikitokea hivyo, mtaondoka na kwenda mahali alipopachagua Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, na huko mtawaendea makuhani Walawi, na mwamuzi aliye kazini wakati huo, nanyi mtatoa mashtaka mbele yao, nao watatoa uamuzi wao. Kisha mtafanya kama watakavyowatangazieni pale mahali Bwana atakapopachagua; mtakuwa waangalifu kufanya yote kama watakavyowaagiza. Itawabidi kufanya kufuatana na maongozi watakayowapatia na uamuzi watakaoutoa kwenu. Msiache kutimiza kwa dhati hukumu watakayowatangazia. Naye mtu asiyejali kumtii kuhani au mwamuzi aliyewekwa hapo kumhudumia Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, au mwamuzi, mtu huyo atauawa. Ndivyo mtakavyokomesha uovu miongoni mwenu. Watu wote watasikia na kuogopa wasifanye tena kitu kwa kutojali.
Kumbukumbu la Sheria 17:8-13 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ikiwa limezuka neno lililo zito kukupita wewe, katika maamuzi kati ya damu na damu, na kati ya kesi na kesi, na kati ya pigo na pigo, nayo yashindaniwa katika malango yako; ndipo nawe uondoke, ukwee uende mahali atakapochagua BWANA, Mungu wako; uwaendee makuhani Walawi, na mwamuzi atakayekuwako siku hizo; uwaulize; nao watakuonesha hukumu ya maamuzi; nawe fanya sawasawa na hukumu watakayokuonesha mahali hapo atakapochagua BWANA; nawe tunza kufanya kwa mfano wa yote watakayokufunza; kwa mfano wa sheria watakayokufunza, na kwa mfano wa hukumu watakayokuambia, fanya vivyo hivyo; usigeuke katika hukumu watakayokuonesha, kwenda mkono wa kulia wala wa kushoto. Na mtu afanyaye kwa kujikinai, kwa kutomsikiza kuhani asimamaye hapo kwa kumtumikia BWANA, Mungu wako, au mwamuzi, na afe mtu huyo; nawe utauondoa uovu katika Israeli. Na hao watu wote watasikia na kuogopa, wasifanye tena kwa kujikinai.
Kumbukumbu la Sheria 17:8-13 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ikiwa limezuka neno lililo zito kukupita wewe, katika maamuzi kati ya damu na damu, na kati ya daawa na daawa, na kati ya pigo na pigo, nayo yashindaniwa katika malango yako; ndipo nawe uondoke, ukwee uende mahali atakapochagua BWANA, Mungu wako; uwaendee makuhani Walawi, na mwamuzi atakayekuwako siku hizo; uwaulize; nao watakuonyesha hukumu ya maamuzi; nawe fanya sawasawa na hukumu watakayokuonyesha mahali hapo atakapochagua BWANA; nawe tunza kufanya kwa mfano wa yote watakayokufunza; kwa mfano wa sheria watakayokufunza, na kwa mfano wa hukumu watakayokuambia, fanya vivyo; usigeuke katika hukumu watakayokuonyesha, kwenda mkono wa kuume wala wa kushoto. Na mtu afanyaye kwa kujikinai, kwa kutomsikiza kuhani asimamaye hapo kwa kumtumikia BWANA, Mungu wako, au mwamuzi, na afe mtu huyo; nawe utauondoa uovu katika Israeli. Na hao watu wote watasikia na kuogopa, wasifanye tena kwa kujikinai.
Kumbukumbu la Sheria 17:8-13 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Kama mashauri yanaletwa katika mahakama zenu ambayo ni magumu zaidi kwenu kuyaamua, ikiwa ni umwagaji wa damu, madai au mashambulio, yapelekeni mahali Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, atakapopachagua. Nendeni kwa makuhani, ambao ni Walawi, na kwa mwamuzi ambaye atakuwa kazini wakati huo. Ulizeni kwao nao watawapa maamuzi. Ni lazima mtende sawasawa na maamuzi watakayowapa mahali Mwenyezi Mungu atakapopachagua. Kuweni waangalifu kufanya kila kitu watakachowaongoza kufanya. Fanyeni sawasawa na sheria wanayowafundisha na maamuzi wanayowapa. Msigeuke mkono wa kuume au kushoto kuacha kufanya yale wanayowaambia. Mwanaume atakayeonesha dharau kwa mwamuzi au kwa kuhani ambaye amewekwa kumtumikia Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, lazima auawe. Lazima mwondoe uovu katika Israeli. Watu wote watasikia na kuogopa, nao hawatakuwa wenye kudharau tena.