Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Wathesalonike Utangulizi

Utangulizi
Paulo katika safari yake ya pili kueneza Injili alitembelea mji wa Thesalonike, ambao ulikuwa kituo cha biashara. Alihudumu huko kwa majuma matatu, akahubiri katika sinagogi la Wayahudi, akithibitisha kutoka Maandiko Matakatifu kwamba Isa ndiye Al-Masihi. Baadhi ya Wayahudi na Wayunani wakaamini, lakini ilimlazimu Paulo kuondoka huko haraka kwa sababu ya upinzani mkubwa uliozuka humo.
Baada ya kufika Athene, Paulo alipata habari kutoka kwa Timotheo kuwa ingawa walipata mateso, waumini wa Thesalonike walikuwa wamesimama imara. Paulo aliandika barua hii ili kuwatia moyo na kuwafariji waumini waliokuwa wachanga katika Al-Masihi. Aliwaandikia ili kuimarisha imani yao kuhusu maisha yale mfuasi wa Al-Masihi anapaswa kuishi, na pia kuhusu kurudi kwa Isa. Yamkini waumini hawa walikuwa na wasiwasi kwamba wafuasi wa Al-Masihi wenzao waliokuwa wamekufa hawangeweza kuufikia ufufuo wa wafu. Hivyo Paulo akawaandikia kuwahakikishia kwamba waliokufa wakiwa wanamwamini Al-Masihi watafufuka kwanza.
Mwandishi
Mtume Paulo.
Kusudi
Kuwaimarisha wafuasi wa Al-Masihi wa Thesalonike katika imani yao, na kuwapa hakikisho kuhusu kurudi kwa Isa.
Mahali
Korintho.
Tarehe
Mnamo 51 B.K.
Wahusika Wakuu
Paulo, Timotheo na Silvano.
Wazo Kuu
Kuwatia waumini moyo kudumu katika utakatifu, na kuwahakikishia wale wanaoteswa kwamba Mwenyezi Mungu yu pamoja nao na amewaahidi ushindi.
Mambo Muhimu
Paulo aliwaandikia Wathesalonike barua hii ili kuwatia moyo na kuwafariji katika Al-Masihi, na pia kuimarisha imani yao katika misingi ya mafundisho ya Al-Masihi.
Yaliyomo
Salamu na shukrani za Paulo (1:1-10)
Huduma ya Paulo Thesalonike, na matukio tangu kuondoka Thesalonike (2:1–3:13)
Mwenendo na maisha ya kumcha Mwenyezi Mungu (4:1-12)
Kurudi kwake Bwana Isa (4:13–5:11)
Maagizo ya mwisho, na hitimisho (5:12-28).

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia