1 Wafalme Utangulizi
Utangulizi
Katika maandiko ya Kiebrania, vitabu vya 1 Wafalme na 2 Wafalme vilikuwa kitabu kimoja kilichoitwa “Wafalme” katika mapokeo ya Kiyahudi. Huku kutenganishwa kwa vitabu hivi kulifanywa na watafsiri wa Maandiko Matakatifu kwa Kiyunani linaloitwa “Septuagint” na vikatambulishwa kama “Kitabu cha Tatu na cha Nne cha Ufalme.” Vitabu vya Samweli na Wafalme vinaelezea historia yote kuhusu ufalme wa Israeli, vile ulivyoinuka wakati wa Samweli, na vile ulivyoanguka mikononi mwa Wababeli.
Mwandishi
Mwandishi wa kitabu hiki hajulikani, lakini mapokeo ya Kiyahudi yanasema mwandishi ni nabii Yeremia, au kikundi cha manabii.
Kusudi
Kulinganisha maisha ya wale waliomwishia Mwenyezi Mungu na wale waliokataa kumwishia Mwenyezi Mungu, kupitia historia ya wafalme wa Israeli na Yuda.
Mahali
Katika nchi ya Israeli.
Tarehe
Wakati kitabu hiki kiliandikwa haujulikani.
Wahusika Wakuu
Daudi, Sulemani, Rehoboamu, Yeroboamu, Ilya, Ahabu na Yezebeli.
Wazo Kuu
Kugawanyika kwa Israeli kuwa falme mbili: Ufalme wa Kaskazini uliojulikana kama Israeli, ambao ulikuwa na makabila kumi, na Ufalme wa Kusini uliojulikana kama Yuda, ambao ulikuwa na makabila mawili.
Mambo Muhimu
Kifo cha Daudi, utawala wa Sulemani, kujengwa kwa Hekalu, kugawanyika kwa ufalme, na huduma ya Ilya.
Yaliyomo
Utawala wa Sulemani (1:1–11:43)
Rehoboamu na Yeroboamu (12:1–14:31)
Wafalme wa Israeli na Yuda (15:1–16:34)
Ilya na Ahabu (17:1–19:21)
Utawala wa Ahabu na Yezebeli (20:1–22:53).
Iliyochaguliwa sasa
1 Wafalme Utangulizi: NENO
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
![None](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2F58%2Fhttps%3A%2F%2Fweb-assets.youversion.com%2Fapp-icons%2Fsw.png&w=128&q=75)
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Neno: Maandiko Matakatifu™ NMM™
Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc.
Imetumiwa kwa ruhusa.
Haki zote zimehifadhiwa duniani kote.
Kiswahili Contemporary Scriptures™
Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Used with permission. All rights reserved worldwide.