1 Wakorintho 10:12-14
1 Wakorintho 10:12-14 NEN
Hivyo, yeye ajidhaniaye amesimama, aangalie asianguke. Hakuna jaribu lolote lililowapata ambalo si la kawaida kwa wanadamu. Naye Mungu ni mwaminifu; hataruhusu mjaribiwe kupita mnavyoweza. Lakini mnapojaribiwa atawapa njia ya kutokea ili mweze kustahimili. Kwa hiyo wapenzi wangu, zikimbieni ibada za sanamu.