1 Nyakati 9
9
1Waisraeli wote waliorodheshwa katika koo zilizoandikwa kwenye kitabu cha wafalme wa Israeli.
Wakazi wa Yerusalemu
Watu wa Yuda walichukuliwa mateka kwenda Babeli kwa sababu ya kukosa uaminifu kwa Mungu.
2Basi watu wa kwanza kurudi kukaa kwenye milki zao katika miji yao walikuwa baadhi ya Waisraeli, makuhani, Walawi na watumishi wa Hekalu#9:2 yaani Wanethini.
3Wale waliotoka Yuda, Benyamini, Efraimu na Manase ambao waliishi Yerusalemu walikuwa:
Jamaa za Yuda
4Uthai mwana wa Amihudi, mwana wa Omri, mwana wa Imri, mwana wa Bani, wa wana wa Peresi, mwana wa Yuda.
5Wazao wa Washiloni waliorudi ni:
Asaya mzaliwa wa kwanza na wanawe.
6Kwa wana wa Zera:
Yeueli.
Watu wa Yuda jumla yao walikuwa watu mia sita na tisini (690).
Jamaa za Benyamini
7Kwa Benyamini walikuwa:
Salu mwana wa Meshulamu, mwana wa Hodavia, mwana wa Hasenua;
8Ibneya mwana wa Yerohamu,
Ela mwana wa Uzi, mwana wa Mikri;
na Meshulamu mwana wa Shefatia, mwana wa Reueli, mwana wa Ibniya.
9Watu kutoka Benyamini, kama walivyoorodheshwa katika koo zao, jumla yao walikuwa mia tisa na hamsini na sita (956). Watu hawa wote walikuwa viongozi wa jamaa zao.
Jamaa za makuhani
10Wa jamaa za makuhani walikuwa:
Yedaya, Yehoyaribu na Yakini;
11Azaria mwana wa Hilkia, mwana wa Meshulamu, mwana wa Sadoki, mwana wa Merayothi, mwana wa Ahitubu aliyekuwa afisa kiongozi wa nyumba ya Mungu.
12Adaya mwana wa Yerohamu, mwana wa Pashuri, mwana wa Malkiya;
Maasai, mwana wa Adieli, mwana wa Yahzera, mwana wa Meshulamu, mwana wa Meshilemithi, mwana wa Imeri.
13Makuhani waliokuwa viongozi wa jamaa zao walikuwa elfu moja na mia saba na sitini (1,760). Walikuwa watu wenye uwezo, waliowajibika kuhudumu katika nyumba ya Mungu.
Jamaa za Walawi
14Jamaa za Walawi walikuwa:
Shemaya, mwana wa Hashubu, mwana wa Azrikamu, mwana wa Hashabia, wa wana wa Merari.
15Bakbakari, Hereshi, Galali na Matania mwana wa Mika, mwana wa Zikri, mwana wa Asafu.
16Obadia mwana wa Shemaya, mwana wa Galali, mwana wa Yeduthuni.
Berekia mwana wa Asa, mwana wa Elkana, ambao waliishi katika vijiji vya Wanetofathi.
Jamaa za mabawabu
17Mabawabu katika Hekalu la Mwenyezi Mungu waliorudi walikuwa:
Shalumu, Akubu, Talmoni, Ahimani na ndugu zao. Shalumu alikuwa mlinzi wao mkuu. 18Walikuwa wamewekwa katika lango la mfalme lililokuwa upande wa mashariki, hadi wakati huu. Hawa walikuwa mabawabu kutoka kambi ya Walawi.
19Shalumu mwana wa Kore, mwana wa Ebiasafu, mwana wa Kora, pamoja na mabawabu wenzake kutoka jamaa yake ya Kora waliwajibika kulinda malango ya Hema, kama baba zao walivyokuwa wamewajibika kulinda ingilio la Maskani ya Mwenyezi Mungu.
20Hapo zamani Finehasi mwana wa Eleazari alikuwa kiongozi wa mabawabu, naye Mwenyezi Mungu alikuwa pamoja naye:
21Zekaria mwana wa Meshelemia alikuwa bawabu katika ingilio la Hema la Kukutania.
22Jumla ya waliochaguliwa kuwa mabawabu katika sakafu za kupuria nafaka walikuwa watu mia mbili na kumi na wawili (212). Waliandikishwa kwa koo zao kwenye vijiji vyao.
Mabawabu hawa waliwekwa katika nafasi zao za kuaminiwa na Daudi, pamoja na Samweli aliyekuwa mwonaji. 23Wao na wazao wao walikuwa viongozi wa kulinda malango ya nyumba ya Mwenyezi Mungu, nyumba iliyoitwa Hema. 24Mabawabu walikuwa pande zote nne: mashariki, magharibi, kaskazini na kusini. 25Ndugu zao katika vijiji vyao walikuwa wakija mara kwa mara, na kuwasaidia katika kazi zao kwa vipindi mbalimbali vya siku saba. 26Lakini mabawabu wanne wakuu, waliokuwa Walawi, walikabidhiwa wajibu wa kusimamia vyumba na hazina katika nyumba ya Mungu. 27Walikesha mahali walipowekwa kuizunguka nyumba ya Mungu, kwa sababu iliwapasa kuilinda. Pia walitunza funguo kwa ajili ya kufungua mlango kila siku asubuhi.
28Baadhi yao walikuwa viongozi wa kutunza vifaa vilivyotumika katika huduma ndani ya Hekalu; walivihesabu kila vilipoingizwa ndani na kila vilipotolewa. 29Wengine walipangiwa kutunza mapambo na vifaa vingine vya patakatifu, pamoja na unga, divai, mafuta, uvumba na vikolezo. 30Lakini baadhi ya makuhani walifanya kazi ya kuchanganya vikolezo. 31Mlawi aliyeitwa Matithia, mwana mzaliwa wa kwanza wa Shalumu, wa ukoo wa Kora, alikabidhiwa wajibu kwa ajili ya kuoka mikate ya sadaka. 32Baadhi ya ndugu zao wa koo za Wakohathi walikuwa viongozi wa kuandaa mikate ya Wonesho kwa ajili ya kila Sabato, mikate iliyokuwa inawekwa mezani.
33Wale waliokuwa waimbaji, viongozi wa jamaa za Walawi, waliishi katika vyumba vya Hekalu, nao hawakufanya shughuli nyingine yoyote kwa sababu iliwapasa kuwajibika kwa kazi hiyo usiku na mchana.
34Hawa wote walikuwa viongozi wa jamaa za Walawi, wakuu kama walivyoorodheshwa katika koo zao, nao waliishi Yerusalemu.
Ukoo wa Sauli
(1 Nyakati 8:29-38)
35Yeieli alikuwa baba yake Gibeoni, naye aliishi huko Gibeoni.
Mke wake aliitwa Maaka, 36mwanawe mzaliwa wa kwanza alikuwa Abdoni, akafuatiwa na Suri, Kishi, Baali, Neri, Nadabu, 37Gedori, Ahio, Zekaria na Miklothi. 38Miklothi akamzaa Shimeamu. Wao pia waliishi karibu na jamaa zao huko Yerusalemu.
39Neri akamzaa Kishi, Kishi akamzaa Sauli. Sauli akamzaa Yonathani, Malki-Shua, Abinadabu na Esh-Baali.#9:39 au Ish-Boshethi, maana yake Mtu wa Aibu (2 Samweli 2:8)
40Yonathani akamzaa Merib-Baali#9:40 au Mefiboshethi,
naye Merib-Baali akamzaa Mika.
41Wana wa Mika walikuwa:
Pithoni, Meleki, Tarea, na Ahazi.
42Ahazi akamzaa Yara, Yara akawazaa Alemethi, Azmawethi na Zimri, naye Zimri akamzaa Mosa. 43Mosa akamzaa Binea, Binea akamzaa Refaya, na mwanawe huyo ni Eleasa, na mwanawe huyo ni Aseli.
44Aseli alikuwa na wana sita, na haya ndiyo majina yao:
Azrikamu, Bokeru, Ishmaeli, Shearia, Obadia na Hanani. Hao walikuwa wana wa Aseli.
Iliyochaguliwa sasa
1 Nyakati 9: NENO
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Neno: Maandiko Matakatifu™ NMM™
Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc.
Imetumiwa kwa ruhusa.
Haki zote zimehifadhiwa duniani kote.
Kiswahili Contemporary Scriptures™
Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Used with permission. All rights reserved worldwide.