Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Nyakati 8

8
Ukoo wa Sauli Mbenyamini
1Benyamini akamzaa:
Bela mzaliwa wake wa kwanza,
Ashbeli mwanawe wa pili, Ahara mwanawe wa tatu,
2Noha mwanawe wa nne na Rafa mwanawe wa tano.
3Wana wa Bela walikuwa:
Adari, Gera, Abihudi, 4Abishua, Naamani, Ahoa, 5Gera, Shefufani na Huramu.
6Hawa ndio wazao wa Ehudi, waliokuwa viongozi wa jamaa za wale walioishi huko Geba na ambao walihamishiwa Manahathi:
7Naamani, Ahiya na Gera. Gera ndiye aliwapeleka uhamishoni, na alikuwa baba yao Uza na Ahihudi.
8Shaharaimu aliwazaa wana katika nchi ya Moabu baada ya kuwapa talaka wake zake wawili yaani Hushimu na Baara. 9Kwa mkewe Hodeshi, akawazaa wana saba: Yobabu, Sibia, Mesha, Malkamu, 10Yeuzi, Sakia na Mirma. Hao walikuwa wanawe, viongozi wa jamaa zao. 11Hushimu alimzalia: Abitubu na Elpaali.
12Wana wa Elpaali walikuwa:
Eberi, Mishamu, Shemedi (aliyeijenga miji ya Ono na Lodi, pamoja na vijiji vyake), 13na Beria na Shema, waliokuwa viongozi wa zile jamaa zilizokuwa zinaishi katika mji wa Aiyaloni, na ambao waliwafukuza wenyeji wa Gathi.
14Wana wa Beria walikuwa Ahio, Shashaki, Yeremothi, 15Zebadia, Aradi, Ederi, 16Mikaeli, Ishpa, na Yoha.
17Zebadia, Meshulamu, Hizki, Heberi, 18Ishmerai, Izlia na Yobabu ndio walikuwa wana wa Elpaali.
19Yakimu, Zikri, Zabdi, 20Elienai, Silethai, Elieli, 21Adaya, Beraya na Shimrathi walikuwa wana wa Shimei.
22Wana wa Shashaki walikuwa Ishpani, Eberi, Elieli, 23Abdoni, Zikri, Hanani, 24Hanania, Elamu, Anthothiya, 25Ifdeya na Penueli.
26Shamsherai, Sheharia, Athalia, 27Yaareshia, Ilya na Zikri walikuwa wana wa Yerohamu.
28Hawa wote walikuwa viongozi wa jamaa zao wakuu, kama walivyoorodheshwa katika koo zao, nao waliishi Yerusalemu.
29Yeieli alikuwa baba yake Gibeoni naye aliishi huko Gibeoni.
Mke wake aliitwa Maaka. 30Mwanawe mzaliwa wa kwanza alikuwa Abdoni, akafuatiwa na Suri, Kishi, Baali, Neri, Nadabu, 31Gedori, Ahio, Zekeri, 32na Miklothi aliyekuwa baba yake Shimea. Hawa pia waliishi karibu na jamaa zao huko Yerusalemu.
33Neri akamzaa Kishi, Kishi akamzaa Sauli, Sauli akamzaa Yonathani, Malki-Shua, Abinadabu na Esh-Baali.
34Yonathani akamzaa:
Merib-Baali#8:34 au Mefiboshethi, maana yake Mtu wa Aibu (taz. 2 Samweli 4:4)., naye Merib-Baali akamzaa Mika.
35Wana wa Mika walikuwa:
Pithoni, Meleki, Tarea na Ahazi.
36Ahazi akamzaa Yehoada. Naye Yehoada akawazaa Alemethi, Azmawethi na Zimri, naye Zimri akamzaa Mosa. 37Mosa akamzaa Binea; Refaya alikuwa mwanawe Binea, Eleasa mwanawe Refaya, naye Aseli mwanawe Eleasa.
38Aseli alikuwa na wana sita; haya ndiyo majina yao:
Azrikamu, Bokeru, Ishmaeli, Shearia, Obadia na Hanani. Hawa wote ndio walikuwa wana wa Aseli.
39Wana wa Esheki, nduguye Aseli, walikuwa:
Mzaliwa wake wa kwanza alikuwa Ulamu, wa pili Yeushi na wa tatu Elifeleti. 40Wana wa Ulamu walikuwa mashujaa hodari walioweza kutumia upinde. Alikuwa na wana wengi na wajukuu, jumla yao mia moja na hamsini.
Hawa wote ndio walikuwa wazao wa Benyamini.

Iliyochaguliwa sasa

1 Nyakati 8: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia