1 Nyakati 7
7
Wana wa Isakari
1Wana wa Isakari walikuwa:
Tola, Pua, Yashubu na Shimroni; wote ni wanne.
2Wana wa Tola walikuwa:
Uzi, Refaya, Yerieli, Yahmai, Ibsamu na Samweli waliokuwa viongozi wa jamaa zao. Wakati wa utawala wa Mfalme Daudi, wazao wa Tola walioorodheshwa kama wapiganaji katika ukoo wao walikuwa watu elfu ishirini na mbili na mia sita.
3Mwana wa Uzi alikuwa:
Izrahia.
Wana wa Izrahia walikuwa:
Mikaeli, Obadia, Yoeli na Ishia. Wote hawa watano walikuwa wakuu wao. 4Kulingana na ukoo wa jamaa zao, walikuwa na watu elfu thelathini na sita waliokuwa wamejiandaa kwa vita, kwa sababu walikuwa na wanawake na watoto wengi.
5Jamaa waliokuwa wapiganaji kutoka koo zote za Isakari, kama walivyoorodheshwa katika ukoo wao, walikuwa elfu themanini na saba.
Wana wa Benyamini
6Wana watatu wa Benyamini walikuwa:
Bela, Bekeri na Yediaeli.
7Wana wa Bela walikuwa:
Esboni, Uzi, Uzieli, Yerimothi na Iri; walikuwa viongozi wa jamaa zao; wote ni watano. Wapiganaji walioorodheshwa katika ukoo wao walikuwa elfu ishirini na mbili na thelathini na wanne (22,034).
8Wana wa Bekeri walikuwa:
Zemira, Yoashi, Eliezeri, Elioenai, Omri, Yeremothi, Abiya, Anathothi na Alemethi. Hawa wote walikuwa wana wa Bekeri. 9Orodha ya ukoo wao iliyoandikwa viongozi wa jamaa zao walikuwa wapiganaji elfu ishirini na mia mbili.
10Mwana wa Yediaeli alikuwa:
Bilhani.
Wana wa Bilhani walikuwa:
Yeushi, Benyamini, Ehudi, Kenaana, Zethani, Tarshishi na Ahishahari. 11Hawa wana wote wa Yediaeli walikuwa viongozi wa jamaa zao. Kulikuwa na wapiganaji elfu kumi na saba na mia mbili waliokuwa tayari kwa vita.
12Washupimu na Wahupimu walikuwa wazao wa Iri. Wahushimu walikuwa wazao wa Aheri.
Wana wa Naftali
13Wana wa Naftali walikuwa:
Yahzieli, Guni, Yeseri na Shalumu; hao walikuwa wazao wa Bilha.
Wana wa Manase
14Wazao wa Manase walikuwa:
Asirieli alikuwa mzao wake kutokana na suria wake Mwaramu. Huyu suria akamzaa Makiri baba wa Gileadi. 15Makiri akatwaa mke kutoka miongoni mwa Wahupimu na Washupimu. Jina la dada yake Makiri aliitwa Maaka. Mwana mwingine wa Makiri aliitwa Selofehadi, aliyekuwa na watoto wa kike tu. 16Maaka mkewe Makiri akamzaa mwana aliyemwita Pereshi. Jina la nduguye lilikuwa Shereshi. Wana wa Pereshi walikuwa Ulamu na Rakemu.
17Mwana wa Ulamu alikuwa:
Bedani.
Hao walikuwa wana wa Gileadi mwana wa Makiri, mwana wa Manase.
18Dada yake aliyeitwa Hamolekethi aliwazaa Ish-Hodi, Abiezeri na Mahla.
19Wana wa Shemida walikuwa:
Ahiani, Shekemu, Liki na Aniamu.
Wana wa Efraimu
20Wazao wa Efraimu walikuwa:
Shuthela, ambaye alimzaa Beredi,
Beredi akamzaa Tahathi, Tahathi akazaa Eleada,
Eleada akamzaa Tahathi, 21Tahathi akamzaa Zabadi,
na Zabadi akamzaa Shuthela.
Ezeri na Eladi waliuawa na wenyeji wa Gathi walipokuwa wameenda huko kuwanyang’anya mifugo yao. 22Baba yao Efraimu akawaombolezea kwa siku nyingi, na jamaa zake wakaja kumfariji. 23Kisha akakutana kimwili na mke wake tena, naye akachukua mimba, akamzalia mwana. Akamwita jina Beria, kwa sababu ya misiba iliyoipata nyumba yake. 24Beria alikuwa na binti jina lake Sheera. Huyu ndiye aliijenga miji ya Beth-Horoni ya Juu na Beth-Horoni ya Chini, pamoja na Uzen-Sheera.
25Beria akamzaa pia Refa, naye Refa akamzaa Reshefu,
Reshefu akamzaa Tela, Tela akamzaa Tahani,
26Tahani akamzaa Ladani, Ladani akamzaa Amihudi,
Amihudi akamzaa Elishama, 27Elishama akamzaa Nuni,
Nuni akamzaa Yoshua.
28Nchi zao na makazi yao yalijumuisha Betheli na vijiji vilivyouzunguka, Naarani ilikuwa upande wa mashariki, Gezeri pamoja na vijiji vyake upande wa magharibi, pia Shekemu na vijiji vyake hadi kufikia Aya na vijiji vyake. 29Katika mipaka ya Manase kulikuwa na Beth-Shani, Taanaki, Megido na Dori pamoja na vijiji vyake. Wazao wa Yusufu mwana wa Israeli waliishi katika miji hii.
Wana wa Asheri
30Wana wa Asheri walikuwa:
Imna, Ishva, Ishvi na Beria. Dada yao alikuwa Sera.
31Wana wa Beria walikuwa:
Heberi na Malkieli, aliyekuwa baba yake Birzaithi.
32Heberi akawazaa Yafleti, Shomeri na Hothamu, na Shua dada yao.
33Wana wa Yafleti walikuwa:
Pasaki, Bimhali na Ashvathi.
Hawa walikuwa wana wa Yafleti.
34Wana wa Shemeri walikuwa:
Ahi, Roga, Yehuba na Aramu.
35Wana wa Helemu ndugu yake walikuwa:
Sofa, Imna, Sheleshi na Amali.
36Wana wa Sofa walikuwa:
Sua, Harneferi, Shuali, Beri, Imra, 37Bezeri, Hodu, Shama, Shilsha, Ithrani#7:37 au Yetheri na Beera.
38Wana wa Yetheri walikuwa:
Yefune, Pispa na Ara.
39Wana wa Ula walikuwa:
Ara, Hanieli na Risia.
40Hawa wote ndio walikuwa wazao wa Asheri, viongozi wa jamaa zao, watu bora, mashujaa hodari na viongozi maarufu. Idadi ya watu waliokuwa wamejiandaa kwa vita, kama walivyoorodheshwa katika ukoo wao, walikuwa elfu ishirini na sita.
Iliyochaguliwa sasa
1 Nyakati 7: NENO
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Neno: Maandiko Matakatifu™ NMM™
Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc.
Imetumiwa kwa ruhusa.
Haki zote zimehifadhiwa duniani kote.
Kiswahili Contemporary Scriptures™
Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Used with permission. All rights reserved worldwide.