1 Nyakati 6
6
Wana wa Lawi
1Wana wa Lawi walikuwa:
Gershoni, Kohathi na Merari.
2Wana wa Kohathi walikuwa:
Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli.
3Amramu alikuwa na wana:
Haruni, Musa, na Miriamu.
Haruni alikuwa na wana:
Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari.
4Eleazari akamzaa Finehasi,
Finehasi akamzaa Abishua,
5Abishua akamzaa Buki,
Buki akamzaa Uzi,
6Uzi akamzaa Zerahia,
Zerahia akamzaa Merayothi,
7Merayothi akamzaa Amaria,
Amaria akamzaa Ahitubu,
8Ahitubu akamzaa Sadoki,
Sadoki akamzaa Ahimaasi,
9Ahimaasi akamzaa Azaria,
Azaria akamzaa Yohanani,
10Yohanani akamzaa Azaria (ndiye alifanya kazi ya ukuhani katika Hekalu alilojenga Mfalme Sulemani huko Yerusalemu),
11Azaria akamzaa Amaria,
Amaria akamzaa Ahitubu,
12Ahitubu akamzaa Sadoki,
Sadoki akamzaa Shalumu,
13Shalumu akamzaa Hilkia,
Hilkia akamzaa Azaria,
14Azaria akamzaa Seraya,
Seraya akamzaa Yehosadaki.
15Yehosadaki alihamishwa wakati Mwenyezi Mungu aliwapeleka uhamishoni watu wa Yuda na Yerusalemu kwa mkono wa Mfalme Nebukadneza.
16Wana wa Lawi walikuwa:
Gershoni, Kohathi na Merari.
17Haya ndiyo majina ya wana wa Gershoni:
Libni na Shimei.
18Wana wa Kohathi walikuwa:
Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli.
19Wana wa Merari walikuwa:
Mahli na Mushi.
Zifuatazo ni koo za Walawi wakiorodheshwa kufuatana na baba zao:
20Wazao wa Gershoni:
Gershoni akamzaa Libni, Libni akamzaa Yahathi,
Yahathi akamzaa Zima, 21Zima akamzaa Yoa,
Yoa akamzaa Ido, Ido akamzaa Zera,
Zera akamzaa Yeatherai.
22Wazao wa Kohathi:
Kohathi akamzaa Aminadabu, Aminadabu akamzaa Kora,
Kora akamzaa Asiri, 23Asiri akamzaa Elkana,
Elkana akamzaa Ebiasafu, Ebiasafu akamzaa Asiri,
24Asiri akamzaa Tahathi, Tahathi akamzaa Urieli,
Urieli akamzaa Uzia, Uzia akamzaa Shauli.
25Wazao wa Elkana walikuwa:
Amasai na Ahimothi,
26Ahimothi akamzaa Elkana, Elkana akamzaa Sofai,
Sofai akamzaa Nahathi, 27Nahathi akamzaa Eliabu,
Eliabu akamzaa Yerohamu, Yerohamu akamzaa Elkana,
Elkana akamzaa Samweli.
28Wana wa Samweli walikuwa:
Yoeli mzaliwa wake wa kwanza,
na Abiya mwanawe wa pili.
29Wafuatao ndio wazao wa Merari:
Merari akamzaa Mahli, Mahli akamzaa Libni,
Libni akamzaa Shimei, Shimei akamzaa Uza,
30Uza akamzaa Shimea, Shimea akamzaa Hagia,
Hagia akamzaa Asaya.
Waimbaji wa Hekalu
31Hawa ndio watu ambao Daudi aliwaweka kuwa viongozi wa uimbaji katika nyumba ya Mwenyezi Mungu, baada ya Sanduku la Agano kuletwa ili kukaa huko. 32Walihudumu kwa kuimba mbele ya Maskani, Hema la Kukutania, hadi hapo Mfalme Sulemani alipojenga Hekalu la Mwenyezi Mungu huko Yerusalemu. Walitimiza wajibu wao kulingana na taratibu walizokuwa wamewekewa.
33Wafuatao ni watu waliohudumu pamoja na wana wao:
Kutoka koo za Wakohathi walikuwa:
Hemani, mpiga kinanda,
alikuwa mwana wa Yoeli, mwana wa Samweli,
34mwana wa Elkana, mwana wa Yerohamu,
mwana wa Elieli, mwana wa Toa,
35mwana wa Sufu, mwana wa Elkana,
mwana wa Mahathi, mwana wa Amasai,
36mwana wa Elkana, mwana wa Yoeli,
mwana wa Azaria, mwana wa Sefania,
37mwana wa Tahathi, mwana wa Asiri,
mwana wa Ebiasafu, mwana wa Kora,
38mwana wa Ishari, mwana wa Kohathi,
mwana wa Lawi, mwana wa Israeli;
39na msaidizi wa Hemani alikuwa Asafu, aliyesimama mkono wa kuume:
Asafu mwana wa Berekia, mwana wa Shimea,
40mwana wa Mikaeli, mwana wa Baaseya,
mwana wa Malkiya, 41mwana wa Ethni,
mwana wa Zera, mwana wa Adaya,
42mwana wa Ethani, mwana wa Zima,
mwana wa Shimei, 43mwana wa Yahathi,
mwana wa Gershoni, mwana wa Lawi.
44Na kutoka kwa walioshirikiana nao, Wamerari, mkono wake wa kushoto:
Ethani mwana wa Kishi, mwana wa Abdi,
mwana wa Maluki, 45mwana wa Hashabia,
mwana wa Amazia, mwana wa Hilkia,
46mwana wa Amzi, mwana wa Bani,
mwana wa Shemeri, 47mwana wa Mahli,
mwana wa Mushi, mwana wa Merari,
mwana wa Lawi.
48Ndugu zao wengine Walawi walipewa huduma nyingine za kuhudumia hema takatifu, nyumba ya Mungu.
49Lakini Haruni na uzao wake ndio walikuwa na wajibu wa kutoa sadaka katika madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa na kwenye madhabahu ya kufukizia uvumba pamoja na yote yaliyofanyika pa Patakatifu, wakifanya upatanisho kwa ajili ya Israeli, sawasawa na yale yote aliyoagiza Musa mtumishi wa Mungu.
50Hawa walikuwa wazao wa Haruni:
Haruni akamzaa Eleazari, Eleazari akamzaa Finehasi,
Finehasi akamzaa Abishua, 51Abishua akamzaa Buki,
Buki akamzaa Uzi, Uzi akamzaa Zerahia,
52Zerahia akamzaa Merayothi, Merayothi akamzaa Amaria,
Amaria akamzaa Ahitubu, 53Ahitubu akamzaa Sadoki,
Sadoki akamzaa Ahimaasi.
54Zifuatazo ni sehemu walizopewa ziwe nchi yao kwa ajili ya makazi yao (walipewa wazao wa Haruni waliotoka katika ukoo wa Wakohathi, kwa sababu kura ya kwanza iliwaangukia):
55Walipewa Hebroni katika nchi ya Yuda pamoja na maeneo ya malisho yanayouzunguka. 56Lakini mashamba pamoja na vijiji vilivyouzunguka mji alipewa Kalebu mwana wa Yefune. 57Kwa hiyo wazao wa Haruni walipewa miji ifuatayo: Hebroni (mji wa makimbilio), Libna, Yatiri, Eshtemoa, 58Hileni, Debiri, 59Ashani, Yuta na Beth-Shemeshi pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji.
60Kutoka kabila la Benyamini, walipewa Gibeoni, Geba, Alemethi na Anathothi, pamoja na maeneo yake ya malisho.
Miji hii kumi na tatu iligawanywa miongoni mwa koo za Wakohathi.
61Wazao waliobaki wa Wakohathi walipewa miji kumi kutoka koo za nusu ya kabila la Manase.
62Wazao wa Gershoni, kufuatana na koo zao, walipewa miji kumi na tatu kutoka kwa makabila ya Isakari, Asheri na Naftali, na kutoka sehemu ya kabila la Manase huko Bashani.
63Wazao wa Merari, kufuatana na koo zao walipewa miji kumi na mbili kutoka makabila ya Reubeni, Gadi na Zabuloni.
64Kwa hiyo Waisraeli waliwapa Walawi miji hii pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji.
65Kutoka makabila ya Yuda, Simeoni na Benyamini walipewa miji iliyotajwa hapo juu.
66Baadhi ya koo za Wakohathi walipewa kama nchi yao miji kutoka kabila la Efraimu.
67Katika nchi ya vilima ya Efraimu, walipewa Shekemu (mji wa makimbilio) na Gezeri, 68Yokmeamu, Beth-Horoni, 69Aiyaloni na Gath-Rimoni, pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji.
70Kutoka nusu ya kabila la Manase, Waisraeli waliwapa koo za Wakohathi waliobaki miji ya Aneri na Bileamu pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji.
71Wagershoni walipokea miji ifuatayo:
Katika nusu ya kabila la Manase, walipokea Golani katika Bashani, na pia Ashtarothi, pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji.
72Kutoka kabila la Isakari walipokea Kedeshi, Daberathi, 73Ramothi na Anemu, pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji.
74Kutoka kabila la Asheri, walipokea Mashali, Abdoni, 75Hukoki na Rehobu, pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji.
76Kutoka kabila la Naftali, walipokea Kedeshi katika Galilaya, Hamoni na Kiriathaimu, pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji.
77Wamerari (Walawi waliobakia) walipokea miji ifuatayo:
kutoka kabila la Zabuloni, walipokea Yokneamu, Karta, Rimoni na Tabori, pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji.
78Kutoka kabila la Reubeni, ng’ambo ya Yordani mashariki mwa Yeriko, walipokea Bezeri ulioko jangwani, Yahasa, 79Kedemothi na Mefaathi, pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji.
80Na kutoka kabila la Gadi, walipokea Ramothi huko Gileadi, Mahanaimu, 81Heshboni na Yazeri, pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji.
Iliyochaguliwa sasa
1 Nyakati 6: NENO
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Neno: Maandiko Matakatifu™ NMM™
Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc.
Imetumiwa kwa ruhusa.
Haki zote zimehifadhiwa duniani kote.
Kiswahili Contemporary Scriptures™
Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Used with permission. All rights reserved worldwide.