Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Nyakati 4

4
Koo nyingine za Yuda
1Wazao wa Yuda walikuwa:
Peresi, Hesroni, Karmi, Huri na Shobali.
2Reaya mwana wa Shobali akamzaa Yahathi, Yahathi akawazaa Ahumai na Lahadi. Hizo zilikuwa koo za Wasorathi.
3Hawa walikuwa wana wa Etamu:
Yezreeli, Ishma na Idbashi. Dada yao aliitwa Haselelponi. 4Penueli akamzaa Gedori, naye Ezeri akamzaa Husha.
Hawa walikuwa wazao wa Huri, mzaliwa wa kwanza wa Efrata, na baba yake Bethlehemu.
5Ashuri baba yake Tekoa alikuwa na wake wawili, Hela na Naara.
6Hawa walikuwa wazao wa Naara: Ahuzamu, Heferi, Temeni na Haahashtari.
7Wana wa Hela walikuwa:
Serethi, Sohari, Ethnani, 8na Kosi ambaye aliwazaa Anubi, Sobeba na jamaa zote za Aharheli mwana wa Harumu.
9Yabesi aliheshimiwa kuliko ndugu zake. Mama yake alimwita Yabesi, akisema, “Nilimzaa kwa huzuni.” 10Yabesi akamlilia Mungu wa Israeli akisema, “Ee Mungu, laiti ungenibariki kweli na kuipanua mipaka yangu! Mkono wako na uwe pamoja nami, uniepushe na uovu ili nisidhurike!” Naye Mungu akamjalia hayo aliyoyaomba.
11Kelubu, nduguye Shuha, akamzaa Mehiri, naye Mehiri akamzaa Eshtoni. 12Eshtoni akawazaa Beth-Rafa, Pasea na Tehina. Tehina alikuwa baba wa Iri-Nahashi. Hao walikuwa wazao wa Reka.
13Wana wa Kenazi walikuwa:
Othnieli na Seraya.
Wana wa Othnieli walikuwa:
Hathathi na Meonothai. 14Meonothai akamzaa Ofra.
Seraya akamzaa Yoabu,
baba wa Ge-Harashimu#4:14 maana yake Bonde la Mafundi, lililoitwa hivyo kwa sababu watu walioishi humo walikuwa mafundi stadi.
15Kalebu mwana wa Yefune alikuwa na wana watatu:
Iru, Ela na Naamu.
Naye mwana wa Ela alikuwa:
Kenazi.
16Wana wa Yahaleleli walikuwa:
Zifu, Zifa, Tiria na Asareli.
17Wana wa Ezra walikuwa:
Yetheri, Meredi, Eferi na Yaloni.
Mmoja wa wake zake Meredi aliwazaa: Miriamu, Shamai na Ishba aliyekuwa baba yake Eshtemoa. 18Hawa walikuwa watoto wa Bithia binti Farao, ambaye Meredi alikuwa amemwoa.
Meredi alikuwa na mke mwingine wa kabila la Yuda ambaye aliwazaa: Yeredi baba wa Gedori, Heberi baba wa Soko, na Yekuthieli baba wa Zanoa.
19Wana wa mke wa Hodia aliyekuwa dada yake Nahamu walikuwa:
baba yake Keila, Mgarmi na Eshtemoa, Mmaakathi.
20Wana wa Shimoni walikuwa:
Amnoni, Rina, Ben-Hanani na Tiloni.
Wazao wa Ishi walikuwa:
Zohethi na Ben-Zohethi.
21Wana wa Shela, mwana wa Yuda, walikuwa:
Eri baba yake Leka, Laada baba yake Maresha na jamaa za wafumaji nguo za kitani safi walioishi huko Beth-Ashbea,
22Yokimu, watu walioishi Kozeba, Yoashi na Sarafi waliotawala huko Moabu na Yashubi-Lehemu. (Taarifa hizi ni za zamani sana.) 23Hawa walikuwa wafinyanzi walioishi Netaimu na Gedera; waliishi huko wakimtumikia mfalme.
Simeoni
24Wazao wa Simeoni walikuwa:
Nemueli, Yamini, Yaribu, Zera na Shauli.
25Mwana wa Shauli alikuwa Shalumu, Shalumu akamzaa Mibsamu, na Mibsamu akamzaa Mishma.
26Wazao wa Mishma walikuwa:
Hamueli aliyemzaa Zakuri, Zakuri akamzaa Shimei.
27Shimei alikuwa na wana kumi na sita, na binti sita, lakini ndugu zake hawakuwa na watoto wengi, hivyo ukoo wao wote haukuwa na watu wengi kama ukoo wa Yuda. 28Waliishi Beer-Sheba, Molada, Hasar-Shuali, 29Bilha, Esemu, Toladi, 30Bethueli, Horma, Siklagi, 31Beth-Markabothi, Hasar-Susimu, Beth-Biri na Shaaraimu. Hii ilikuwa miji yao hadi wakati wa utawala wa Daudi. 32Vijiji vya miji hiyo vilikuwa Etamu, Aini, Rimoni, Tokeni na Ashani: miji mitano, 33pamoja na vijiji vyote kuizunguka miji hii hadi huko Baali.
Haya yalikuwa makazi yao. Nao waliweka kumbukumbu ya ukoo wao:
34Meshobabu, Yamleki,
Yosha mwana wa Amazia, 35Yoeli,
Yehu mwana wa Yoshibia, mwana wa Seraya, mwana wa Asieli.
36Pia Elioenai, Yaakoba, Yeshohaya,
Asaya, Adieli, Yesimieli, Benaya,
37Ziza mwana wa Shifi, mwana wa Aloni, mwana wa Yedaya, mwana wa Shimri, mwana wa Shemaya.
38Watu hawa walioorodheshwa hapa juu kwa majina walikuwa viongozi wa koo zao.
Jamaa zao ziliongezeka sana, 39wakaenea wakafika viunga vya Gedori kuelekea mashariki mwa bonde wakitafuta malisho kwa ajili ya mifugo yao. 40Huko walipata malisho mengi mazuri, nayo nchi ilikuwa na nafasi kubwa, yenye amani na utulivu. Baadhi ya Wahamu walikuwa wameishi huko awali.
41Watu walioorodheshwa majina walikuja nchi hiyo wakati wa Hezekia mfalme wa Yuda. Wasimeoni wakawashambulia Wahamu katika makao yao pamoja na Wameuni ambao walikuwa huko, nao wakawaangamiza kabisa, kama ilivyo dhahiri hadi leo. Kisha wakaishi huko kwa sababu kulikuwa na malisho mazuri kwa mifugo yao. 42Watu wa kabila la Simeoni wapatao mia tano, wakiongozwa na Pelatia, Nearia, Refaya na Uzieli wana wa Ishi, wakavamia nchi ya vilima ya Seiri. 43Wakawaua Waamaleki waliobaki, na waliokuwa wamenusurika; nao wanaishi huko hadi leo.

Iliyochaguliwa sasa

1 Nyakati 4: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia